STARTING A BUISNESS AT YOUNG AGE and DEVELOPING ENTREPRENEURSHIP SPIRIT/KUANZA BIASHARA KATIKA UMRI MDOGO NA KUENDELEZA DHIMA YA UJASIRIAMALI.
STARTING
A BUISNESS AT YOUNG AGE and DEVELOPING ENTREPRENEURSHIP SPIRIT/KUANZA BIASHARA
KATIKA UMRI MDOGO NA KUENDELEZA DHIMA YA UJASIRIAMALI.
Nini maana ya Biashara ? zipo
maana nyingi sana kama
▶Biashara
ni kitendo cha kununua na kuuza bidhaa mbalimbali
▶Biashara
inaweza kuwa utekelezaji wa wazo fulani kwa namna ambayo unapata pesa katika
hiyo
Biashara na ujasiriamali ni vitu
viwili katika fungu moja
Mjasiriamali ni
▶
mtu anayechukua hatua za utekelezaji wa wazo kwa nia ya kupata fedha
▶Mmiliki
wa biashara anayefanya kazi huku akikabiliana na Changamoto mbali mbali kwa
juhudi kubwa (He takes initiatives dispite the Risk))
▶
Mjasiriamali ni mtu anayekuwa tayari kuanzisha biashara na kuwa tayari
kuwajibika kwa kila hali na yuko tayari kwa matokeo yoyote
▶Ni
mtu anayekuwa tayari kuanza upya hata biashara inapokwama na hata kufa kabisa
anatulia anajitathmini kisha anaanza tena.
Na ujasiriamali ni kitendo cha
kuchukua hatua na kisha kuanza hiyo biashara. Hasa kwa lengo la kupata
fedha na kutatua matatizo ya watu.
KUTATUA MATATIZO YA WATU
KWANINI NI MUHIMU KUANZA BIASHARA AU
UJASIRIAMALI KATIKA UMRI MDOGO.
Tunaona katika
▶
Maombolezo 3:27
Ni vema mwanadamu aichukue nira
Wakati wa ujana wake.
Hivyo ni vyema kufanya maamuzi na
kuanza katika ujana ili hata ukikutana na changamoto unakuwa na nafasi ya kuzitatua
maana umri wako bado unakupa nafasi ya kufanya mambo mengi zaidi .Kumbuka
NGUVU ZAKO NI MTAJI WAKO zitumie kwa hekima
▶Ujasiriamali
hausubiri umri fulani wala hauangalii jinsia Fulani, hivyo huna kikwazo cha
kuanza sasa amka chukua hatua.
Mithali 20:29
Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na
uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.
kuna msemo unaosema
WAKATI SAHIHI WA KUOTESHA MTI
ULIKUWA MIAKA ISHIRINI ILIYOPITA....... WAKATI MWINGINE SAHIHI NI SASA.
(The best time to plant a tree was
20 years ago. The second best time is now)
▶Ukiwa
kijana ni rahisi kujifunza maarifa na ujuzi kwa haraka zaidi kuliko ukiwa
mzee .
▶Ukiwa
na umri mdogo inakupa nafasi ya kuweza kushindana na ushindani wa soko la
biashara husika maana kwa asilimia kubwa Utahusika moja kwa moja katika
biashara yako.
▶
Inaweza kukupa nafasi ya kuwa mgunduzi wa kwanza wa unachokifanya
▶Inakupa
nafasi ya kuwa mtoa ajira badala ya kuwa mtafuta ajira
▶
Ukianza katika umri mdogo inakupa nafasi ya kustaafu mapema ukiwa bado una nguvu
kwa sababu umeanza mapema na umewekeza vya kutosha kukutunza ukiwa mzee.
▶Unaweza
kujenga misingi mizuri ya familia na ngome ya nyumbani kwako mapema
NAMNA YA KUANZA BIASHARA KATIKA UMRI
MDOGO
v Challenge yourself
~Jiulize je ninaweza .??
~hivi ninapenda kujiajiri au
kuajiriwa?
~hata kama nimeajiriwa ni vipi
nitatengeneza kipato nje ya mshahara wangu?
v Engage your Gift / passion
Husisha karama yako au kile kitu
unaona unapenda na unasikia amani ukikifanya na kinakupa furaha
*Turn your passion into
profit*
v Take Risk
Mara nyingi tunaogopa kuanza kwa
kuogopa matokeo ni wazi kuwa huwezi kuona matokeo bila kuamua kuanza,Jipe moyo
mkuu ANZA LEO
v Believe in yourself
Vijana wengi tunakatishwa tamaa na
maneno ya watu kwamba hatuwezi hatuwezi .Hebu leo ongea na nafsi yako
jiambie NINAWEZA NA NINAYAWEZA YOTE KWAKUWA NINAE YESU ANAYENIPA UWEZO. Hii
itakusaidia hata ukipata changamoto usikate tamaa maana STUMBLING BLOCKS ARE
STEPING STONES
v Find the right association
Jihusianishe na watu husika kwa kile
unachotaka kufanya Mfano. Ninataka kufungua Pharmacy watu husika ni walio
kwenye mchepuo wa dawa au tiba kwa binadamu nikienda kuuliza changamoyo kwa
watu wenye hoteli haitakuwa sahihi kwangu. Tafuta mkondo sahihi wa
uelekeo wa Wazo lako kisha anza.
v Have a mentor
Ni muhimu sana kuwa na
mwangalizi ,Mwangalizi wa hali yako ya kiroho ila pia mwangalizi wa hali
yako ya maisha na hatua zako , Na hakikisha unamwambia kwa uwazi kila
unachoona anapaswa kujua .
atakusaidia ,
Atakushauri,
Atakufundisha,
Ataku councel,
Atakukosoa pia
Ila pia Mentor
..Will help you to see Further
..Will help you to move faster
..Will help you to easy gain
strength and overcome weakness
They are you are support base
YOU NEED A MENTOR
Wewe kama mjasiriamali inabidi uwe na uwezo wa
kujiamini kwasababu hatujapewa roho ya woga
2 timotheo 1:7
Maana Mungu hakutupa roho ya woga,
bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Wajasiriamali wengi tunaowaona
hawakuanza moja kwa moja
Walianza wakaanguka wakasimama
wakaanza tena na leo tunawajua kwa majina NEVER GIVE UP
Lazima mjasiriamali uwe na tabia ya
kuwatia moyo wengine ili waweze kusimama kwasababu hata sisi tunaye
aliyetuwezesha
1 wakorinto 2:16
Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya
Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
Kila unapotaka kuanza ukaona kama
huwezi sema I HAVE THE MIND OF CHRIST ,mimi ninayo nia ya Kristo Hii
itakupa ujasiri wa kusonga .Usisahau kabisa hili, mjasiriamali hachoki
kutafuta maarifa na ujuzi hata atakapofanikiwa
Mwanzo 26:18_25[18]Isaka akarudi
akavichimbua vile visima vya maji walivyovichimba siku za Ibrahimu babaye;
maana wale Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kufa kwake Ibrahimu; naye
akaviita majina kufuata majina alivyoviita babaye.[19]Watumwa wa Isaka
wakachimba katika lile bonde, wakapata kisima cha maji yanayobubujika.[20]Wachungaji
wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka wakisema, Maji haya ni yetu. Ndipo
akakiita jina la kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye.[21]Wakachimba
kisima kingine, wakagombania na hicho tena. Akakiita jina lake Sitna. [22]Akaondoka
huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake
Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi
katika nchi. [23]Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba.[24]BWANA akamtokea
usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana
mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya
Ibrahimu mtumishi wangu. [25]Akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Akapiga hema yake huko, na watumwa wa Isaka wakachimba kisima huko.
Hivi ndivyo tunavyopaswa kuwa hakuna
kukata tamaaa
Ukishindwa leo unajaribu kesho,Ukikosa
hivi inajaribu vile Usiwe na mipaka katika utendaji kwasababu UNAYAWEZA *YOTE*
KATIKA YEYE ATUTIAYE NGUVU.Ukiona akili inakwambia inatosha sema hapana naweza
kufanya tena kidogo hicho kidogo cha ziada kitaleta utofauti Ukikatishwa tamaa
usijali,
Sio lazima ukubalike sokoni moja kwa
koja unachotakiwa kufanya ni
KUWA WA TOFAUTI na UTOFAUTI Mfano.
duka A na B wanauza mikate ila duka A... mikate yao huwa ni milaini na inahifadhiwa
katika hali nzuri na safi Duka B...mikate yao ni migumu na inafungwa kwenye magazeti
tuu yaliyotumika tayari.Wewe ukitaka mkate utaenda wapi??
_Kuwa wa tofauti kwa kufanya
kitu cha tofauti_
Hivyo kijana wa Kikristo unapowaza kuwa
mjasiriamali kumbuka UNAYO NIA YA KRISTO na kikubwa ni kumuhusisha katika kila
jambo Kisha tulia fanya maamuzi sahihi, Sio kila wanachofanya wengine
wakapata pesa unatakiwa ukifanye.
YOU ARE IN A MISSION WITH CHRIST
eee Kumbuka fedha yako ina sehemu utatoa Zaka ,Malimbuko,Fungu la kumi ,hivyo
hakikisha unaipata kwa namna inayompendeza Mungu ili iwe manukato mbele
zake .Turn your vision into a mission Ila pia hakikisha UNATOA SAPPORT KWA
WAJASIRIAMALI WENGINE
HITIMISHO
Katika kuwaza kwako fikiria jambo
kubwa ili ikishindikana ufanye kidogo chenye tija
Ukiwaza kidogo ikashindikana basi
utakosa kabisa cha kufanya.
( GO BIG OR GO HOME)
An entrepreneur
dont aim to play small
_Aim high reach higher_
Imetafsiriwa na Dada Vick Mcharo.
No comments