DEALING WITH MENTAL AND EMOTION ISSUES / KUJIHUSISHA NA MASWALA YA AFYA YA AKILI NA MIHEMKO
DEALING
WITH MENTAL AND EMOTION ISSUES /
KUJIHUSISHA NA MASWALA YA AFYA YA
AKILI NA MIHEMKO
Tukianza na Emotion ni hisia ambazo
mtu anakuwa nazo kama
kuwa na furaha au huzuni,Hizi mbili
zinaelezeka kwa namna nyingi tofautii
Hisia zinapelekea mambo mengi kama
kuwa na msongo wa mawazo,,kuwa na kiwewe (Anxiety) kuwa na hasira au
furaha. Mara nyingi zinasababishwa na matukio ambayo tumepitia katika maisha
kama kufiwa na wapendwa wetu, kuvunjika kwa mahusiano kuyumba kiuchumi kufeli kwenye
maisha na nyingine nyingi
Matatizo haya yanawapata zaidi
vijana hasa ni depression na anxiety
Na wengi wakikosa muongozo sahihi
wakati huu wanakuwa na tabia hasi kama kujitenga na baadae wengi hufikiria na
hata hujaribu kujiua.
Rekodi ya shirika la afya
duniani WHO mwaka 2018 inaonyesha watu zaidi ya 800,000 hujiua kila mwaka
kutokana na matatizo haya ya msongo wa mawazo.
Ila tukumbuke kuwa Emotions (
MIHEMKO) ni Hazina kubwa
Hii inakufanya uwe jinsi ulivyo. Unafahamu
kuwa YESU pia alikuwa na emotion? Tunaona Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na
tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na
ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi.
Sababu pekee inayopelekea tuwe na
mihemko ni kwasababu MUNGU mwenyewe ambaye ametuumba kwa mfano wake alikuwa
nazo na aliziweka ndani yetu tangu uumbwaji ili tuhusiane sisi kwa sisi na sisi
na yeye Mungu
Hivyo sio kitu kibaya. Lakini
pia tunaona Yesu alikuwa na emotions aliona huruma,alikasirika pia Mathayo
9:36Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na
kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.
Wakati Mungu anahangaika au
anashughulikia maisha yetu kuna namna tunatakiwa kuishi na kuna vitu vya
kuepuka.
1. Emotionalism.
( kuendeshwa na Mihemko)
Ni hali ya kusema kitu kikubwa
kwenye maisha ni kujali vile ninavyojisikia whats matters is how I feel
▶Haijalishi
nini ninafikiria
▶Haijalishi
kipi ni sahihi
▶Haijalishi
kipi sio sahihi
Ninachojali ni namna
ninajisikia
HII NI HALI YA KUEPUKA
KWASABABU MUNGU ANATAKA TUMSHIRIKISHE KILA KITU SI TUJALI HISIA ZETU BALI
TUWEZE KUMSIKIA KATIKAKTI YA HISIA ZETU
Hivyo epuka kusema
❌❌I DO WHAT I FEEL LIKE DOING❌❌
Bali kwa sisi tuliokombolewa na
Kristo EVERY THING MATTERS
2. STOICISM
Feelings au hisia ni jambo
zuri ila stoicism ni kinyume chake
Ni hali ya kuona hisia hazima maana
yoyote. Na hii ndio maana mara nyingi hisia zetu zinakuwa ni ubinafsi, Hivyo hili
pia ni jambo la kuzingatia sana tunapo deal na mental au emotions issues
Ni muhimu kujua hisia zako na hisia za wengine pia nini mahusiano ya hisia
zako na watu wengine na Mungu.
Ila pia Mungu ametupa hisia kwa
kusudi maalum
Je unafahamu kuwa Mungu anataka
tumuabudu katika uhalisia wa HISIA zetu( worship him emotionally)
Na ndio maana maandiko yanasema mara
nyingi kuwa wananiamudu kwa midomo yao ila nafsi zao ziko mbali na mimi
Kwa maana nyingine ni kwamba unakuwa
kimwili ila KIHISI haupo hapo
Mathayo 15:8 Watu hawa huniheshimu
kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.Mungu anatazamia hisia zetu zihusike
katika kumuabudu,Uwepo wako wakati unatafuta uwepo wake
Pia maandiko yanasema katika Mathayo
33:37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako
yote, na kwa akili zako zote.
HITIMISHO
HAKIKISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU
UNAKUWA HAI WAKATI WOTE ILI ROHO WA MUNGU AFANYE KAZI NDANI YAKO
ATAKUPA TUNDA LA ROHO MTAKATIFU
▶love
▶joy
▶peace
▶patience
▶kindness
▶goodness
▶faithfulness
▶gentleness
▶SELF
CONTROL
Galatia 5::22
Lakini tunda la Roho ni upendo,
furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
[23 upole, kiasi; juu ya mambo
kama hayo hakuna sheria.
Bwana Yesu atusaidie ili tuweze
kujua namna ya kudeal na hizi situation
▶USIJICHUKIE
▶USIMCHUKIE
WA KUMKASIRIKIA MUNGU
▶
KAMA UKIJUA SABABU YA DEPRESSION LET IT
GO
KWASABABU SIKU ZOTE MSAMAHA
UNATUSAIDIA KWANZA
SO LET IT GO FORGIVE YOURSELF THEN
MOVE ON
1.Feelings are often unreliable(
mara nyingi hisia HAZIAMINIKI)
▶
Zinaweza kukupeleka katika uelekeo mwingine
ni mara ngapi umedhani UNAJUA kumbe
haujui?
Umewaza hili ni jambo sahihi
ninafanya kumbe sio
umehisi kitu fulani ni haki yako
kumbe sio ?
Hii inaonyesha dhahiri hisia sio
ZAKUAMINIKA mara zote.
Mara nyingine tunawaamini watu kumbe
HAWA AMINIKI tuone
2 Samweli 13 Tunaona habari za
Amnoni na Tamari namna ambavyo Amnoni aliaminiwa kumbe hakufaa kuaminiwa mwisho
wa siku alimbaka umbu lake Tamari
Mithali 14:12 Iko njia
ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti. Kila
wakati kabla hujaamua hebu kaa chini tulia fikiria kisha sema
2. To please God /Kumpendeza Mungu
Namna tunavyomuona Mungu mioyoni
mwetu ndivyo tunavyopata nafasi ya kumuheshimu Mungu hawezi kuongoza maisha
yetu kama hisia zinaongoza maisha yetu
Warumi 8:6-8[6]Kwa kuwa nia ya mwili
ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.[7]Kwa kuwa ile nia ya mwili ni
uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu,wala haiwezi kuitii.[8]Wale
waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
3.To succeed in life (
kufanikiwa katika maisha )
Neno linasema Roho akiwaongoza hamko
chini ya sheria.Hivyo kufanikiwa ni rahisi kwa kanuni za kimungu
HOW TO MANAGE EMOTIONAL ISSUES
1. Iainishe na uitaje kwa
jina ,Ili kushughulika na tatizo ni lazima ulijue kwanza
2. Challenge it
Ukishaijua kuwa shida inayonisumbua
ni hii ipe changamoto
mfano
▶Unajisikia
huzuni kwa ajili ya jambo fulani Jiulize
o
Hili
jambo ni kweli au la?? Naweza kulihandle au laaa?
o
wakati
mwingine unaweza mshirikisha rafiki akupe changamoto juu ya hilo jambo
o
Pata
mtu ambaye unaweza kumueleza mambo yako yote ili akushauri
o
Hakikisha
hawa watu sio wale wa kusema ndio kwa kila kitu au pole na akaishia hapo
au duu kweli hii ni cchangamoto akaishia hapo .Tafuta mtu atakaye
kuchallenge na kukushauri
Zaburi 26:2
Ee BWANA, unijaribu na kunipima;
Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.
3. Tame it by changing it
Jiulize mood yako inaweza
kudumu kwa muda gani?
Unaweza kuibadili kwa
kufikiria vitu vingine tofauti na unachofanya sasa
Wafilipi2:5
Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu
ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
Imetafsiriwa na Dada Vick Mcharo
Imetafsiriwa na Dada Vick Mcharo
No comments