MAISHA YA WOKOVU KWA KIJANA.
Ninakusalimu
katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.Ninapenda kumshukuru Mungu kwa kutupatia
neema ya kujifunza somo hili ambalo limekuja kwa wakati sahihi la WOKOVU KWA
VIJANA WAKRISTO. Miaka ya nyuma kidogo watu alikuwa wanaufahamu finyu au mdogo wa
neno la Mungu na kwanzia mdogo hata mkubwa wote waliamini kuwa wokovu ulikuwa
ni kwa ajili ya wazee ambao wanasubiria kuondoka duniani. Na hata kwenye baadhi
ya nchi zilizoendelea katika nymba za ibada huwa wanaonekana wazee mara zote
kuliko vijana na hii inatuonyesha dhahiri kuwa bado vijana hawajamfahamu muumba
wao na hawajawekewa mazingira ya kujua kuwa imewapasa kuokoka wakati huu wakiwa
bado wana nguvu na wasisubirie wakati wa uzee kwani hata uzee huo wanaweza
wasiufikie ili kumpa Yesu maisha kama isemavyo 1Yohana 2;14b Ninawaandikia
vijana kwa sababu mna nguvu ,na neno la Mungu linakaa ndani yenu,nanyi
mmemshinda Yule mwovu.
Neno la Mungu pia katika kitabu cha Muhubiri
12;1 bado linamtaka kijana kuwa karibu na Mungu na kuhakikisha anatumia nguvu
zake kwa ajili ya kuujenga ufalme wa Mungu. Mkumbuke muumba wako siku za ujana
wako,kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala hazijakaribia miaka utakaposema
mimi sina furaha katika hiyo. Vijana tuna haja ya kumkumbuka muumba
wetu wakati wa ujana na kumkumbuka Muumba wetu ni kwa kumpa Yesu kristo maisha,
kuuishia wokovu na utakatifu.
MAMBO YA
KUZINGATIA
1.KUMPOKEA NA
KUMKUBALI YESU MAISHANI MWAKO.
Ni jambo la
kwanza na la muhimu mno kumpokea Y esu Kristo
kuwa mwokozi wako na mfalme ,rafiki ,mtetezi wako na awe namba moja katika
maisha yako. Unapompokea Yesu Kristo maisha yako yatabadilishwa, marafiki ulionao
watabadilika hata hali ya maisha uliyonayo itabadilishwa kabisa na Yesu ambae
yupo ndani yako. Yohana 1;12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kuwa
wana wa Mungu ndio wale waliaminio jina lake”.Na jambo la kushangaza
huyu Yesu wetu alikufa kwa ajili yako na bado anayafuatilia maisha yako
anakusubiri urudi kakwe nay eye yupo tiyari kukupokea jinsi ulivyo. Haijalishi
umechafuka kiasi gani bado Bwana Yesu anataka na anahamu ukiri kwa kinywa chako
na ufungue moyo wako akupokee neno la MUNGU katika Ufunuo 3;20 linasema “Tazama
nasimama mlangoni nabisha ,mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango
nitaingia kwake,nami nitakula pamoja naye na yeye pamoja nami”. Mungu anasema
na wewe kwa namna ya hiyari kwa wakati huu. Ebu usije ukakipoteza kipindi hiki
cha neema na ukaja wakati mbaya ambao utatamani kuokoka lakini utakuwa
umeshachelewa sana,ebu angalia maisha unayoishi wewe kijana na ufanye uamuzi wa
kumpa Yesu maisha yako.
2. KUMWAMINI
YESU.
Baada ya
kumpokea na kumpa nafasi Yesu kristo maishani mwako sasa unapaswa umwamini
katika kitabu cha Yoh 1;12 tuliosoma hapo juu unasema“Bali wote waliompokea aliwapa
uwezo wa kuwa wana wa Mungu ndio wale waliaminio jina lake”. Baada ya
kumpokea na kupewa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu neno la Mungu linasema ndio
wale waliaminio neno lake. Bwana Yesu Kristo ndio neno lenyewe. Ukisoma yohana
1;1 na kuendelea . tunapaswa kumwamini Yeye na kumtegemea peke yake na kuacha
miungu yoyote ile tuliyokuwa tukiiabudu au kuipa mafasi ya Mungu alliye hai
maishani mwetu. Miungu hiyo inaweza kuwa wazazi wetu, marafiki , maisha ya
mahusiano, ajira n.k kitu chochcote kile ulichokuwa unakipa nafasi ya kwanza
badala ya Mungu .Tunapaswa kumoa Yesu nafasi yake anayostahili. Yohana 3:16,” Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee,
bali awe na uzima wa milele” (wokovu) kuna kitu tunajifunza hapa, Kitu
hicho ni lazima kuamini ndipo wokovu upatikane. Kwa sababu hiyo huwezi kupata
wokovu pasipokumuamini Mungu na Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha
yako. Marko 16:16, Aaminiye na kubatizwa ataokoka;
asiyeamini atahukumiwa .
Waefeso 2;19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na
watakatifu, watu wa nyumbani kwake Mungu. Ni maombi yangu umpe Yesu maisha ungali bado kijana.
Uzidi kubarikiwa dada Magreth kwa mafundisho yako
ReplyDelete