Highlights

AN AMBASSADOR OF JESUS



BALOZI WA UFALME WA MUNGU.
Balozi ni mtu anayeakilisha nchi,ufalme, jamii fulani au eneo Fulani  ambapo ni tofauti na eneo muhusika  alipo. Sisi kama wakristo ni mabalozi wa ufalme wa Mungu hapa duniani na baada ya kumpokea Yesu kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu Yoh 1;12 tunakuwa wana wa Mungu, tuna uwakilisha utatu mtakatifu yaani Mungu Baba ,Mungu Mwana na Mungu Roho mtakatifu .
Ø  katika ufalme wa Mungu sisi ni mawakili wa siri za Mungu na wajumbe wake hapa duniani na tunapaswa kuuishi uungu hapa duniani . kwa mwenendo wetu na matendo yetu.
2 wakorinto 5;20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo ,kana kwamba Mungu anaishi kwa vinywa vyetu,twawaomba ninyi kwa ajili ya  Kristo ,mpatanishwe na Mungu.
New International Version
We are therefore Christ's ambassadors, as though God were making his appeal through us. We implore you on Christ's behalf: Be reconciled to God.

New Living Translation
So we are Christ's ambassadors; God is making his appeal through us. We speak for Christ when we plead, "Come back to God!"

English Standard Version
Therefore, we are ambassadors for Christ, God making his appeal through us. We implore you on behalf of Christ, be reconciled to God.

International Standard Version
Therefore, we are the Messiah's representatives, as though God were pleading through us. We plead on the Messiah's behalf: "Be reconciled to God!"

GOD'S WORD® Translation
Therefore, we are Christ's representatives, and through us God is calling you. We beg you on behalf of Christ to become reunited with God.

New American Standard 1977
Therefore, we are ambassadors for Christ, as though God were entreating through us; we beg you on behalf of Christ, be reconciled to God.

American King James Version
Now then we are ambassadors for Christ, as though God did beseech you by us: we pray you in Christ's stead, be you reconciled to God.

American Standard Version
We are ambassadors therefore on behalf of Christ, as though God were entreating by us: we beseech you on behalf of Christ, be ye reconciled to God.

versions hizi zote zimeelezea kwa kina mstari niliouandika kwa Kiswahili. Kwa kingereza imetumika kama representative /ambassadors .Tunamwona mtume Paul akisema kuwa yeye ni wakili /balozi/mjumbe wa Yesu Kristo na anaomba tupatanishwe naye. Mimi pia naungana na mtume paulo ninawasihi mpatanishwe na Mungu. Hii ndio kazi ya balozi anaongea kwa niaba ya Yule aliyemteua kuwa wakili wake katika eneo husika. 

Ø  Sio kila mtu anaweza kuwa wakili wako au balozi wako au mjumbe wako vivyo hivyo sio kila mtu ni wakili wa siri za Mungu . kuna wengine kwa kujua au bila kujua wamejikuta wakimwakilisha shetani hasa vijana wadogo kabisa. Kuna ambao kwanzia utoto wao wamekuwa mawakala wa shetani kwa kutumikishwa bila ridhaa yao, wengine wamerithishwa na wazazi au bibi na babu zao. Hili halikuwa kusudi la Mungu kumwumba mwanadamu. Yeye alimwumba mwanadamu ili amwabudu, amtumikie, na kuitunza bustani. Ambayo alimuweka baada ya kumuumba.

Binadamu ni balozi wa Mungu duniani . Mungu ni ROHO ukisoma yohana 4.24 na ili tuweze kuwasiliana nae hatuna budi kuingia katika ulimwengu wa Roho na kuweza kuuathiri. Sisi tuna mwili na roho ila yeye ana Roho na hayuko kimwili duniani kwa sababu hiyo sisi tunapaswa kumwakilisha kwanzia kimwili kwa sababu tuna miili . tunapaswa kumwakilisha yeye katika Nyanja hizi ;

Kuzitangaza habari za Yesu kila Mara.
Kama balozi wa Yesu tunapaswa kuzitangaza habari zake kwa wale wanaotuzunguka na wakati mwingine tutamani kuwafikia wale walio mbali waweze kuzipata habari zake. Ni muhimu huzingatia kuwa , ili uweze kumuwakilisha mtu iwe ni mahakamani kama mwanasheria ni lazima uwe unajua habari zake za muhimu katka eneo unalomtetea ili hata utakapoulizwa swali lolote kuhusu huyo unaemtetea usije ukapatwa na kigugumizi katika kumwelezea unayemtetea,ili tuwe mawakili wazuri wa YESU tunapaswa kumjua yeye kiundani. Na kumjua Yesu Kristo kiundani unapaswa kusoma  neno la Mungu BIBLIA. Biblia ndio kitabu pekee kinachotupa kumjua Mungu na kumjua Yesu kristo.

Ø  Ili kuweza kufahamu Yesu unapaswa kusoma vitabu vinne vya injili mara kwa mara ili kuweza kuzijua kwa undani habari za Yesu katika vitabu vya MATHAYO, MARKO, LUKA NA YOHANA. ndipo tunaweza kuzijua habari za Yesu kiundani pamoja na marafiki zake .  kamwe hauwezi kumwelezea Yesu kwa ujasiri bila kuwa umesoma vitabu hivi vinne. Na ili kuwafahamu marafiki zake yaani mitume 12 wa Yesu ni lazima usome kitabu cha MATENDO YA MITUME. Ukishakuwa na msingi huu hautaweza kuyumbishwa kwa namna yoyote ile na utaweza kuwavuta watu wengine pia wawe mabalozi wa Yesu.

SIFA ZA BALOZI WA YESU.
Ø  Balozi wa Yesu siku zote hakubali  Yesu aaibike. Atahakikisha anapambana kwa namna yoyote ile na kwa hekima kubwa ili Yesu ashinde. Hapa siongelei katika mabishano ya kijinga yasiyo ya kujenga bali namaanisha anapambana kwa hali na mali aone Yesu anachukua ushindi kwenye Uchumi wake, elimu yake, katika maisha yake ya kiroho hapo mwanzo nimesema ukishaokoka unakuwa balozi wa Yesu.
Ø  Haonyeshi udhaifu wake mbele za watu . Ukishaokoka unavua matendo ya kale na utu wa zamani na kuvaa utu mpya 1 kor 5; 17 unakuwa kiumbe kipya. Tumezoea kuona kuwa kuwa watu wanaofanya uzinzi, ukevi, wizi ndio tunaona ni watenda dhambi na kusahau kuwa kutokufanya jambo lolote la kiroho bila imani ni dhambi, kukata tama, kukasirika na kuwa na hasira kwa muda mrefu. Chuki, majungu , kupenda fedha n.k hizi ni dhambi na udhaifu mkubwa ambao walokole wengi wanao. Unapaswa kumwomba Mungu akupe kuushinda udhaifu wako . Udhaifu huo usiwe kikwazo cha wewe kukua kiroho au kuuona ufalme wa Mungu.  Unaposhidwa kukotrol udhaifu wako utajikuta unashidwa kuwavuta wengine waje kwa Mungu kwani neno la Mungu linasema Matendo yenu mema yamtuze Baba yenu aliye mbinguni.Matendo yetu yanatakiwa yamtukuze baba yetu aliye mbinguni. Pale tunapopost kwenye mitandao ya kijamii maneno ya kukatisha tamaa nay a kuonenyesha kwamba Mungu wako ameshidwa ni kumhuzunisha Mungu wako na kuonesha kuwa hawezi tena. Na shetani anafurahia sana kwa kumpa support na kuthibitisha adharani kuwa kile alichokifanya kimefanikiwa kama alivyopanga kitokee. Usipende kuweka hadharani hisia mbaya unazokuwa unapitia kwa kipindi kichache cha Maisha yako. Ili kukusaidia unapojisikia mpweke, umejeruhika au umeumizwa au umekata tama  huo ndio wakati wako mzuri wa kufunga na kuomba na kuwa karibu sana na Mungu na kumwimbia zaburi za ushindi na kumwomba akuvushe na kukuganga katika hali unazopitia kwani yeye anazijua hali hizo na hautaweza bila msaada wake. Na badala ya kuandika maneno ya kuonyesha kushidwa kwenye mitandao ya kijamii ni muda sasa wa kuuandika ukuu na ushindi unaoenda kuupata kupitia jaribu unalopitia.

Ø  Ushuhudiaji ; tunapaswa kumshuhudia Mungu na kuzitangaza habari zake kwa watu wote , marika yote na rangi zote. Mshuudie yeye, hakuna mtu asije na jambo la kumshuhudia Mungu kuna mambo Mengi sana Mungu amekufanyia katika maisha yako. Huenda ukupitia kipindi kigumu lakini Mungu alikupa upenyo na ukavuka salama. Unapaswa kumshuhudia ili na watu wengine walio katika wakati mgumu wapate faraja na wamwone Mungu katika hili wanayopitia. Na kwa kufanya hivyo utamzalia Mungu matunda. Kama umeokoka na haujaweza kumshuhudia mtu bado haujawa wakili mzuri wa Mungu. Jitahidi na Mungu akusaidie uweze kumshuhudia yeye.

Waefeso 6;20 ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika mnyororo ; hata nipate ujasir katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena . in English
"For which I am an ambassador in bonds: that therein I may speak boldly, as I ought to speak."


Uzidi kubarikiwa

No comments