Highlights

A LADY WITH A PURPOSE.
Kila binti ana ramani au mchoro wa aina ya maisha anayotamani kuyaishi baada ya miaka miwili, mitano, kumi n.k na picha hii iliyo akilini mwa Binti ni mafanikio tuu na wadada wengi wanaamini kufanikiwa kupitia mwanaume mwenye pesa, badala ya kujitahidi kuanza kufanikiwa kabla ya kumpata huyo mwanaume mwenye hela. Ili uonekane kama msaidizi kwake na sio tegemezi. Wadada tunakosea sana katika hili.

Mithali 31:11"MOYO WA MUMEWE HUMWAMINI, WALA HATAKOSA KUPATA MAPATO." Mwanamke anatakiw pia wingize kipato katika familia sio kumgojea mume wake kufanya kila kitu kwa ajili ya familia. mstari wa 16 unasema "HUANGALIA SHAMBA, AKALINUNUA, KWA MAPATO YA MIKONO YAKE HUPANDA MIZABIBU." Binti jifunze kujitegemea na kuwa na bidii ili kufikia malengo yako.

1 comment: