Highlights

BINTI MWENYE JUHUDI KATIKA KUJISHUHULISHA

Binti, ili uwe na furaha inakubidi kuwa mchapakazi. Namaanisha unatakiwa kuweka uvivu kando kabisa. Wanaume awapendi watu watakaokuwa tegemezi kwao. Wanataka binti ambaye atakuwa mstari wa mbele kuwaonesha mahali penye fursa na mahali ambapo wao wataweza kupata kipato nje ya mshahara. Na kuwa chapakazi huku hakuanzii baada ya kuolewa bali kabla ya kuolewa, usilale wakati huu halafu uwe na matarajio makubwa kwamba nikishaolewa ndio nitakuwa chapakazi na nitajituma hapana! Kujituma kunaanza sasa hivi.

Katika Mwanzo 24 tunaona Isaka akitafutiwa mke, na Elezer aliambiwa aende kumtafutia mke kutoka kule walipokuwa wanaishi. Na elezer alisema binti atakayekuja na kunipa maji na ngamia zangu pia huyo atakuwa natoka kwa Bwana na kweli Rebeka alikuja na akampa maji. Tunamuona Rebeka ni kwa jinsi gani alikuwa anajituma na alikuwa mchapakazi ajabu. Kama asingeenda kisimani asingekutana na Eliezer na kama asingeonana naye ni dhahiri kwamba asingekuwa mke wa Isaka. Ni vema binti ukawa unajituma na kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii.
Hakikisha unajishughulisha na kujituma kusaidia kuosha vyombo, kudeki, kupika, kutandika kitanda vizuri, kutoa vyombo mezani baada ya kula n.k. Usijibweteke na kudeka sana, anza kujitegemea kwani wewe unakuja kuwa mama mwenye nyumba yako baada ya muda.

No comments