MAJIRA YA KUJILIWA KWANGU.
MAJIRA YA KUJILIWA KWANGU.
Kwa kila jambo kuna
majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu".(Mhubiri 3:1)
-Mungu anafanya kila kitu
kwa majira yake ktk maisha yetu,tukiangalia Mwanzo 18:10 malaika walimwambia
Sarah atapata mtoto wa kiume majira yaleyale mwaka unaofwata kama alivyoambiwa
na malaika wa Bwana. Mwanzo 21:1 Mungu alitimiza neno lake alilomwambia
Abrahamu kupitia wale malaika,Sara alijifungua mtoto wa kiume sawasawa na neno
la Bwana.
KUJILIWA NI NINI?
Kujiliwa ni nyakati
ambazo Mungu anakuwa halisi katik maisha yetu. Katika maisha ya wakristo wengi
huwa na hizi hatua (Phases) tatu nazo ni
-kabla ya kuokoka.
-Baada ya kuokoka.
-Baada ya kujiliwa na
Mungu.
Tukichambua kila hatua:
-Kabla
ya kuokoka.
Hapa bado mtu
hajampokea Bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.
-Baada ya kuokoka.
Hapa mtu anaamua
kumkabidhi Kristo maisha yake ili awe Bwana na mwokozi wake.Watu wengi huishia
katika stage hii ndio maana unaona mtu ameokoka lakini hamna improvement from
point A to point B ktk maisha yake mfano mafanikio ktk elimu, uchumi n.k
-Baada ya kujiliwa na Mungu.
Kufikia level hii mtu
anahitaji kuwa na mahusiano yenye nguvu au ya ukaribu sana na Mungu k.v
Abrahamu ambaye ni mfano mzuri wa biblia. (Luka 19:41-44) inaonyesha watu wengi
tunaangamia kwa sababu hatujui majira ya kujiliwa kwetu.
N.B Inahitaji mahusiano
ya ukaribu sana na Mungu ili kujua majira ya kujiliwa kwetu.
MAMBO
3 MUHIMU YANAYOHUSIKA KTK KUJILIWA KWETU.
-Mahusiano yetu na
Mungu.
-Meeting point yetu na
Mungu.
-Tabia zetu (Attitude)
1)Mahusiano
yetu na Mungu.
-Mahusiano yoyote yale
huwa na levels (hatua) mfano mzuri k.v Uchumba ambapo watu hao wawili siku moja
hutarajia kufikia level ya ndoa (marriage).
Vilevile kujiliwa kwetu
na Mungu kunategemea mahusiano yetu sisi na yeye (Mungu).
-Kuna level ukifika
hauhitaji kuomba ili Mungu ashuke inatokea automatically. Yohana MT 9:31, Warumi
8:31.
2)
Meeting point yetu na Mungu.
-Ukishalocate your
spiritual point usiiachie as long as una neno la Bwana hapo (Zaburi 46:10) hapo ndipo Mungu atakapoinua
karama yako hapo ndipo utakapopokea muujiza wako na hapo ndipo wengine
watamuona Mungu kupitia yale anayotenda maishani mwako.
-Kuna baadhi ya watu
bado hawajatambua meeting point yao na Mungu hivyo hutoka kanisa moja kwenda
lingine wakilitafuta neno la Mungu,na miujiza hivyo humzuia Mungu kulocate
their spiritual adress na hivyo hawajiliwi na Mungu katika maisha yao.Inatupasa
kumuomba Roho Mtakatifu atuongoze kutafuta meeting point na Mungu.
3)Tabia zetu
(Attitude)
-Kuna tabia nyingine
zinamzuia Mungu kutujilia katika maisha yetu .(Wagalatia 5;19-21),tabia kama
wivu, hasira,fitina,ugomvi,uasherati...n.k.
Inatupasa kujua maeneo
yetu ya udhaifu na kumuomba Mungu atusamehe na kuyaondoa hayo madhaifu yetu ili
aweze kutujilia ktk maisha yetu .Zab 51:1-3.
SWALI
NA JIBU
Nifanye nini ili niweze
kuepukana na hizi attitude
Ukishajua udhaifu wako
ni vema kuwa na tabia ya kuomba toba mbele za Mungu mara kwa mara ili akusaidie
kuepukana nao na pia jiepushe na mazingira yanayokufanya kuwa dhaifu.
-Ukisoma Zaburi ya 51
Mfalme Daudi alijua udhaifu wake na hio ndio sala yake ya toba mbele za
Mungu,mstari wa 3 amesema "maana nimejua mimi makosa yangu na dhambi yangu
i mbele yangu daima".
No comments