UHUSIANO BINAFSI NA ROHO MTAKATIFU.
UHUSIANO BINAFSI NA ROHO MTAKATIFU.
Ninakusalimu
katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Ninapenda kumshukuru Mungu kwa kutupatia
neema ya kujifunza somo hili wiki hii ambalo ni mwendelezo wa somo la juma
lililopita tuliangalia namna roho mtakatifu anavyofanya kazi ndani yetu . Siku
ya leo tunakwenda mbele kidogo na kuona namna gani kijana anaweza kuwa na
uhusiano binafsi na Roho mtakatifu
Maana
ya uhusiano binafsi ni hali ya kuwa na uhusiano wa peke yako kama mtu mmoja au
mtu binafsi na sio kundi la watu au kuwa na ukaribu, undugu wa karibu sana na
Roho mtakatifu. Neno la Mungu linasema
Yohana 14; 16-18 “Nami nitamwomba Baba baba naye atawapa
msaidizi mwingine ili akae nanyi hata milele, ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu
hauwezi kumpokea kwa sababu haumwoni wala haumtambui ;bali ninyi mnamtambua
maana anakaa kwenu ,naye atakuwa ndani yenu. sitawaacha yatima naja kwenu.
Neno la Mungu hapa linatuambia kuwa “…bali ninyi mnamtambua maana anakaa kwenu ,naye atakuwa ndani yenu” neno
la Mungu limetumia nafsi ya wingi kwa sababu alikuwa anaongea na wanafunzi wake
ila Roho mtakatifu anakaa ndani ya mtu binafsi ndio maana neno linasema naye
atakuwa ndani yenu. Akiwa na maana kwamba kila mtu binafsi atakuwa na Roho
mtakatifu.Hii ni ahadi ambayo Yesu Kristo aliitoa kabla ya kupaa kwenda kwa
baba yake kutuandalia makao. Ni ahadi yake kwetu kila mmoja wetu kuwa na Roho
mtakatifu. Baada ya kuokoka unampokea Roho mtakatifu ili aweze kukusaidia
kuishinda dhambi na dunia.
Ni
maombi yangu kila kijana atamani kuwa na uhusiano na Roho mtakatifu kwani
hakuna uhusiano wowote ulio bora kama uhusiano wa mtu binafsi na Roho
mtakatifu. Kijana mkristo anapokuwa na Roho mtakatifu ndani yake hatapata shida
kuitafuta sauti ya Mungu, hatakuwa mbishi katika kuifuata kweli ya Mungu kwani
kwanzia ndani yake atakuwa anaongozwa na sauti ya Mungu Roho Mtakatifu. Na Roho
Mtakatifu anamshuhudia binafsi na anaielewa sauti ya Mungu inayosema nae ndani
yake na anaitii. Vijana wengi na wakristo wengi kwa ujumla wamejikuta
wakihangaika kila kona kutafuta kuisikia sauti ya Mungu kupitia watu wangine na
kusahau kuwa wao pia Mungu anasema nao kupitia Roho Mtakatifu na wanashidwa
kumtii au wanadhania kuwa ni hisia zao tuu au ni mawazo yao. Nakuhakikishia
kuwa hiyo sauti unayoisikia ndani mwako ikisema na wewe ndani yako hiyo ni
sauti ya Mungu Roho Mtakatifu.Isaya 30; 20b-21”…..lakini waalimu wako hawatafichwa
tena, ila macho yako yatawaona waalimu wako,na masikio yako yatawasikia neno
nyuma yako likisema njia ni hii ifuateni……..” Roho mtakatifu ni mwalimu
na kama ilivyo kazi ya mwalimu ni kumwongoza mwanafunzi katika njia ambayo ni
sahihi na pale mwanafunzi anapokosea mwalimu anamwadhibu na vivyo hivyo na Roho
matakifu kama maandiko yanavyosema mwalimu huyu, Roho mtakatifu atatuwa dhahiri
na tutaona utendaji kazi wake kwa macho yetu na kwa masikio yetu tutaisikia
sauti ,sauti ikisema na kutuelekeza njia sahihi ya kuifuata kama mtu binafsi
bila kushinikizwa katika chochote.
Tunapaswa kuwa na Roho Mtakatifu ndani mwetu
kama mtu binafsi. Ile hali na mazoea ambayo wakristo wengi tumekuwa nayo ya
kuamini kuwa Mungu anasema na watumishi wa madhabahuni pakee sio sahihi ila
kila aliyempokea Yesu maishani mwake na kumkiri kwa kinywa chake Roho matakatifu
anakaaa ndani mwake na kama Roho mtakatifu anakaa ndani mwake basi atakuwa
anampa maongozi na maonyo sahihi kutoka kwake binafsi. Na pale Roho mtakatifu
anapokuwa ndani mwako na ikafikia hatua kuwa unamsikia na kukitii kile
anachokushauri basi kutoka hapo inaonyesha namna unavyozidi kukua na kukomaa
kiroho.
Na haya ndio mapenzi ya Mungu anatamani kutuona kunakua kutoka katika
utoto na kuwa watu wazima. Huku ndiko kuukomalia wokovu. Tuna kila sababu ya
kuuimarisha uhusiano wetu na Roho mtakatifu kuliko uhusiano mwingine wowote,
wakristo wa leo tumekuwa kutitumia nguvu nyingi na gharama kubwa sana
kuimarisha uhusiano wetu na watumishi wa Mungu ili kusikia Mungu akisema nasi
kupitia wao sio kwamba nataka kupinga uhusiano huo ila napenda kukwambia
Uhusiano wa kwanza na wa muhimu kuliko mwingine wowote ni uhusiano wako binafsi
na Roho mtakatifu kwa sababu mtumishi wa Mungu hawezi kukuwambia kila kitu
unachopaswa kufanya kwani ana kundi kubwa la kuhudumia. Unaweza ukaona Mungu
amekuacha au amekusahau katika mapito unayokumbana nayo na ukajikuta ukikimbizana
na watumishi wa Mungu kila kona kwa ajili ya kupata msaada lakini usifanikiwe
kwa sababu Mungu atakataka uwe na uhusiano binafsi na yeye na ndipo atakaposema
na wewe. Unapokuwa na uhusiano na Roho mtakatifu atakufunulia mambo mengi sana
yaliyosirini. Na ataweza pia kuwafunulia na watumishi wa Mungu mambo yako na
wakaweza kukusaidia na ukavuka kwa ushujaa mkubwa katika majira unayopitia
No comments