NAMNA GANI ROHO MTAKATIFU ANATENDA KAZI NDANI YANGU.
MAISHA YA KIJANA MKRISTO NA WOKOVU.
Ninakusalimu
katika jina la Yesu Kristo Bwana wetu, kipindi kilichopita tulipitia maisha ya
wokovu ambapo tuliangalia Roho mtakatifu anavyofanya kazi ndani yetu. Siku ya leo
ninatamani kuendelee mbele kidogo na kuangalia kwa kina ni kwa namna gani Roho
mtakatifu anatenda kazi ndani yetu kama watoto wa Mungu.
·
Roho mtakatifu hutupa amani na uhuru. 2
kor 3;17 “Basi ‘Bwana’ ndiye Roho
,walakini alipo Roho wa Bwana ndipo
penye uhuru”.Roho mtakatifu anapokuwa ndani yako ndani yako unakuwa na
uhuru wa kimungu wenye mipaka,uhuru huu unatokea ndani ya mtu mmoja mmoja na
baadae eneo la kijografia linakuwa na uhuru na amani ya Kristo. Kuna watu
wakati wote wanaonekana wana hofu na huzuni na hata ukijaribu kukaa karibu nao
kujua kwa nini wako katika hali hiyo unakosa jibu, jibu ni kuwa hawana Roho wa
Mun gu ndani mwao
·
Kutusaidia kutambua dhambi. Roho
mtakatifu anapofanya makazi ndani mwetu anatushuhudia au anashuhudia ndani
mwetu pale tunapofanya kinyume na mapenzi ya Mungu. Anatupa kukosa amani na
hali ya kujiona mkosaji inakuja kwa kasi sana ndani ya mwamini na hii ni
kumtaka mtu huyo kuacha kabisa kuendelea kutenda hicho alichokuwa anakitenda au
ni kumtaka atubu na kurejea tena kwa Bwana Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi
zake.
·
Anatuwezesha kutubu na kujuta pale
tunapokosea. Roho mtakatifu anatupa kuwa na hali ya majuto ndani yetu na hali
hii inatujia pale tunapotenda dhambi na Roho mtakatifu anapokuwa anakuletea
hali ya majuto ndani yako au anapokuwa anasema na wewe mara nyingi na
ukashupaza shingo yako, sauti hiyo hukaa kimya ndani yake na haitakuwa inasema
na wewe tena, mfano mzuri ni watu wanaofanya matendo ya kikatili na ya kinyama
kama kunyanyasa watu au vitendo vya mauaji ambavyo havina utu na huruma ndani
yake, watu wanaojishughulisha na matendo haya Roho wa Mungu anakuwa hayupo
ndani yao na wamemzimisha kwa kutoisikiliza sauti na maonyo yake 1wathes 5;19
“Msimzimishe Roho.”Roho mtakatifu
anapokushuhudia unapokuwa umefanya jambo ambalo sio sahihi na ukakataa kumtii
mara kwa mara unakuwa umemzimisha roho mtaktifu ndani yako na neno la Mungu
limetutaka tusimzimishe Roho mtakatifu ndani yetu na njia pekee ya
kutokumzimisha ni pale anapokushuhudia kwamba umekosea uwe na majuto na tubu
mbele za Mungu ili usamehewe.
·
Kutusaidia katika kuomba warumi 8;26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu
kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa
kuugua kusikoweza kutamkwa”. Binadamu wote ni dhaifu hatujui kuomba
ipasavyo kwa maana kwamba maombi yetu huwa yana makosa na mapungufu kadha wa
kadha na Roho mtakatifu pekee ndie
anayeweza kutuombea ipasavyo.Yeye anajua mahitaji yetu ya muhimu kwa wakati huo
tunapokuwa tunaomba wakati kwa jinsi ya mwili tunakuwa tunamwomba Mungu vitu
kwa ajili ya kujiinua,kusifiwa na wenzetu na wakati mwingine kwa ajili ya
kuwaumiza wengine ila pale tunapoomba kwa kuhitaji msaada wa roho mtakatifu .
Mungu Roho mtakatifu hutuombea kwa kuugua kusikotamkika na kila haja
tunayohiitaji roho mtakatifu anatusaidia kutuombea na wakati mwingine yale
ambayo shetani amekusudia juu yetu kwa siri kupitia kuomba kwa msaada wa roho
mtakatifu anakusaidia kuzijua hila za adui shetani na kuzikataa kupitia Roho
mtakatifu.
·
Kutuwezesha kuomba kwa muda mrefu.
Unapokuwa na Roho mtakatifu anakufundisha namna ya kuomba na atakuongoza katika
maeneo tofauti tofauti ambayo utaweza kuyaombea wakati hata haukuwa umejiandaa
kuyabeba maeneo au mahitaji hayo katika maombi. Kama kila ukiomba umekuwa
maneno yanakukaukia au wakati mwingine unasahau mambo ya kuombea ebu badilisha
namna yako ya kuomba na anza kuomba kwa kumwalika roho mtakatifu ndani yako awe
kiongozi wako katika kuomba na utaanza kuona kuomba kwako kuna matunda na kuna
mabadiliko ukilinganisha na ulipokuwa unaomba hapo kabla , unapookoka maombi
yako pia yanapaswa kuwa na kupiga hatua sio pale ulipokuwa jana ndio hapo hapo
tukija kesho kutwa tunakukuta hapo, kunapaswa kuwa na matokeo na mabadiliko
chanya kila siku katika wokovu wako na katika maisha yako ya wokovu.
·
Kutupa ushikira na Mungu Ushirika kwa
tafsiri nyingine ni umoja au ukaribu baina ya wahusika au urafiki pale Roho wa
Mungu anapokuwa ndani yako atakusaidia kuweza kuwa na ushirika mzuri na Mungu
Baba na Mungu mwana Yesu kristo.. 2 kor 13;14 Neema ya Bwana wetu Yesu kristo na upendo wa Mungu Baba na ushirika wa
Roho mtakatifu ukae nasi sote sasa na hata milele.
Kwa mawasiliano
zaidi
Simu 0654444433
0624006533
No comments