MAISHA YA KIJANA MKRISTO NA WOKOVU.
MAISHA YA KIJANA MKRISTO NA WOKOVU.
Ninakusalimu
katika jina la Yesu Kristo Bwana wetu, juma lililopita tulipitia maisha ya
wokovu ambapo tuliangalia mambo mawili ambayo ni ya muhimu ya kuzingatia ili
kumpa Yesu maisha. Ambayo ni kumpokea na kumkubali Yesu kama mwokozi wa maisha yako na Kumwamini Yesu kristo.
Siku
ya leo ninatamani kuendelee mbele kidogo na kuangalia kwa kina ni mambo gani
yanatokea pale mtu yeyete anapompokea Yesu kristo maishani mwake.
Roho mtakatifu anakaa ndani yako.
Roho
mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu .Mungu ana nafsi tatu ambazo ni Mungu Baba,
Mungu Mwana (Yesu kristo) na Mungu Roho mtakatifu. Baada ya Bwana Yesu kristo
kukaa na wanafunzi wake baaada ya kufufuka aliwafundisha mambo mengi sana
ambayo wangepaswa kuendelea kuyafanyia kazi ili ufalme wa Mungu uzidi kusonga
mbele. Na kabla Yesu kupaa kwenda mbinguni aliwahaidi wanafunzi wake kuwapa
msaidizi ambaye ni roho mtakatifu ambae atakuwa kiongozi na mwalimu kwao.Yohana
14; 16-18 “Nami nitamwomba Baba baba naye atawapa msaidizi mwingine ili akae nanyi
hata milele, ndiye roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu
haumwoni wala haumtambui ;bali ninyi mnamtambua maana anakaa kwenu ,naye
atakuwa ndani yenu. sitawaacha yatima naja kwenu.”Bwana Yesu asingeweza
kuendelea kukaa na wanafunzi wake kwa muda wote kwani muda wake wa kukaa nao
kimwili ulikuwa tiyari umeshaisha na alipaswa kurudi nyumbani kwa baba yake
yaani Mungu ili kutuandalia makao ya milele baada ya kumaliza kuishi hapa
duniani, kuna maisha mengine tutakwenda kuishi ambapo kuna maeneo mawili ambayo
ni mbinguni na jehamanu. Bwana Yesu amekwenda kutuandalia makao yetu ya kudumu
mbinguni na baada ya kutuandalia mahali atarudi tena kuja kutuchukua, Bwana
Yesu kristo ilibidi amwombe Mungu ili amtume roho mtakatifu kwa ajili ya kupata
maongozi sahihi kutoka kwake.Kuonyesha njia sahihi ya kuendea, kutukumbusha, kutushauri,kutuonya
na kutufundisha kweli yote ya Mungu ambayo tunapaswa kuifahamu katika maisha
yetu. Unapookoka na kumpa Yesu kristo maisha, Roho mtakatifu anafanya makao
ndani yako na akishafanya makao katika maisha yako kila kitu kinakuwa chini ya
maongozi yake, atakuwa anakushauri katika mambo yote na kikubwa zaidi unapokea
Roho saba za Mungu katika maisha yako Isaya 11;2” Na roho ya BWANA atakaa juu yake
,roho ya hekima na ufahamu,roho ya ushauri, uweza ,roho ya maarifa na kumcha Bwana.”
Roho hizi saba za Mungu zitakuwa ndani yako na utendaji wake wa kazi
utadhihirika wazi wazi kwa watu wote kwamba unaye Roho wa Mungu ndani yake. Roho wa Mungu anapoingia
ndani yako anakupa hekima,ufahamu, ushauri, uweza, maarifa na kumcha Bwana.
Unapofanyika mwana wa Mungu kila kitu katika maisha yako kinabadilishwa kabisa
na mambo yote ya zamani yanabatilishwa ,yanaondolewa na unaanza mwanzo mpya
kabisa pamoja na Bwana Yesu .2 kor 5; 17 “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo
amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita tazama Yamekuwa mapya.” Unapompokea Yesu Kristo maishani mwako
unaanza upya na anayetupa nguvu za kuanza upya ni roho mtakatifu ambae atakuwa
anarejeza na kuumba kwa upya kila ambacho adui ameharibu ndani yako wakati
ambao ulikuwa nje ya uwepo wa mungu. Roho wa Mungu anakupa ujasiri ndani yako wa
kuanza upya.
Itaendelea
…………………………………..
No comments