Highlights

HOW TO HANDLE TEENS GROWTH ISSUES/ JINSI YAKUKABILIANA NA MAMBO MBALIMBALI WAKATI WA UJANA.


HOW TO HANDLE TEENS GROWTH ISSUES/ JINSI YAKUKABILIANA NA MAMBO MBALIMBALI WAKATI WA UJANA.


Kwanza kabisa tunajua jinsi gani ujana una mambo mengi.Kila siku kunakuwa na changamoto mpya ya hapa na pale.Changamoto tunazopitia zinaweza kuwa kiuchumi, kiafya, kielimu, changamoto za familia na mengineyo mengi.Wewe ndo unajua lipi unapitia kwa sasa.

Mda mwingine matatizo yanapelekea watu kujinyonga, kutengwa, mimba zisizotarajiwa, msongo wa mawazo, kutojiamini, kujidharahu nk.
Nadhani hamna mtu ambaye hajawahi kupitia changamoto yeyote.
Kila siku tunapitia changamoto za hapa na pale.kuna mda unaweza kutatua changamoto unayopitia au mda mwingine unaona kabisa huwezi unazimia moyo au kukata tamaa kabisa.

Mda mwingine tupo na watu wanaopitia changamoto kama zetu lakini tunashindwa pia kujua ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia.
Kwa kusema hayo zifuatazo ni njia mbalimbali za kuweza kutusaidia kukabiliana na msongo wa mawazoau shida yoyote tunazopitia

1.  Jua kabisa unachopitia kwamba ni cha kawaida. 
Ni shetani tu anajaribu kutumia hisia zako kukuaminisha kwamba unachopitia sio cha kawaida.Anajaribu kukuvuta mahali utakapoharibika zaidi au kupotea zaidi.

2. Don't give up on yourself/ usijikatie tamaa
Ni kweli mda mwingine huwezi kujua kila kitu lakini hupaswi kujikatia tamaa.
Wewe ndo unatakiwa uwe wa kwanza kujipenda,kujitia moyo na kusonga mbele 1Timothy 4:12 
Inasema mtu awaye yeyote yule asiudharahu ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo na katika upendo na imani na usafi.Uwe na imani hata kama unapitia pembamba kuwa na imani na usijikatie tamaa. Unavyojichukulia wewe ndivyo na wengine watakavyokuchukulia.

3. Tambua watu wote wanaokuzunguka sio maadui zako, shetani ndio adui yako. 
Shetani atataka uwaone ni wabaya au hawakuelewi lakini tambua kuwa shetani ndio adui na sio ndugu,jamaa na rafiki ndio adui zako.Anza kupambana na shetani na sio watu.

5. Surround yourself with positive things. 
Mda mwingine tunakwama kwa sababu tumejikita kwwnye mazingira yakuona hasi tuu na sio mazingira chanya. Ni vizuri tukajiweka kwenye mazingira chanya yatakayotupa kuona mbele na sio kurudi nyuma.

6. Chagua jinsi ya ku control maamuzi unayoyafanya na sauti unazozisikiliza
Sio kila sauti ni ya kusikiliza, angalia vizuri unapoanza kusikiliza watu.
Nyingine unaweza ukapotea au ukakua zaidi na pia maamuzi yeyote utakayochagua yachuje mara mbili. Ni vizuri ukashirikisha hata watu au ukaomba Mungu pia akusaidie kuliko kukurupuka.

7. Pia unalopitia leo linakuwa fundisho kwa mwingine kesho au kesho kutwa. Ni vizuri ukipitia changamoto ukaiona kama ni njia ya kumvusha mwingine, usijichukulie kirahisi. 
2Korinto 1:3-4

8. Changamoto uliyopitia inaweza ukaiona haufai tena lakini bado unaweza kujenga future nzuri sana. Kila siku unayopewa ni ya kubadilisha ya jana. Yesu alikufa kwa ajili yako .Amini umekuwa mpya katika Kristo na kuendelea mbele.

Imetafsiriwa na Dada Dorosela Kimaro

No comments