Highlights

HOW TO GET INVOLVED IN MISSIONS/ KUJIHUSISHA NA UMISHENI KAMA KIJANA.


HOW TO GET INVOLVED IN MISSIONS/ KUJIHUSISHA NA UMISHENI KAMA KIJANA.
Mkristo Mmisionari ni yule anayekubali wito wa Yesu Kristo,na kuwapasha watu waliopotea katika ulimwengu wa giza habari njema za Yesu Kristo,nguvu za Mungu alie hai,busara na baraka zitokazo kwa Mungu pia kutii Mamlaka ya Bwana Mungu.Kila mtu ameumbwa na kuwekwa katika eneo husika  lengo ni kutimiza kusudi la Mungu,kazi kubwa tuliyoitiwa ni injili ya Yesu, kutangaza habari njema.
Huna budi kushika eneo linalokuzunguka kwa kufanya utume huu,hii itakutambulisha wewe ni wa Kristo na ni sifa ya Mmisionari/ mtume aliyetumwa na kutii katika kufanya.

WHO IS A MISSIONARY?

Mmisionari ni mfanyakazi na sio msimamizi. Pia ni mtu anayekwenda kwa roho ya Ushindi. Missionary sio kitu kinachoendeshwa na kanisa bali kinaendeshwa na Ufalme wa Mungu.

Mathayo 9:36-38
36Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji. 37 Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. 38 Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

Sisi ndio watenda kazi wa leo katika kuutangaza Ufalme wa Mungu.
 Tunaona hii ni mpango wa Mungu mwenyewe Bwana wa mavuno atufanye kuwa watendakazi hai katika shamba lake.
1 Tim 2:7 Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.

Marko 3:14-15
14 Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri, 15 tena wawe na amri ya kutoa pepo.
 KWANINI TUNAITWA KWENYE UTUME?
1. Sababu Ulimwengu uko kwenye giza unahitaji nuru ya Injili.
1John 5:19 Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.

2. Watu wanauhitaji 
Mathayo 9:36
 Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.

3. Mungu anataka tuprove hekima yake.
Efeso 3:10-11 ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho; kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.

 4 Sababu Muda ni mchache
Yohana 4:35
Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.
Yohana 9:4
Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.

TUNAWEZAJE KUJIHUSISHA NA UMISIONARI?
Ni kwa kutii na kutenda yale yote ya Mungu na mwanawe Yesu Kristo.
Marko 16:15
Yohana 17:18
Yohana 20:21

Mwisho wewe uliyeshinda yakupasa kuwajulisha watu uweza wake na tumaini waliweke kwa Mungu alie hai,kwa kila saa kila wakati kwa uwezo wa Mungu, sababu watu hawataki kusikia habari za Yesu wanataka kumuona Yesu
Marko 16:15
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Imetafsiriwa na Dada Dorosela Kimaro

2 comments: