MAXIMIZING YOUTHFUL SEASON / KUTUMIA VIZURI KIPINDI CHA UJANA
MAXIMIZING YOUTHFUL SEASON / KUTUMIA
VIZURI KIPINDI CHA UJANA
Tukisoma Muhubiri 3:1
Inasema kila jambo lina majira yake.
Na kuna kuna wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
Kulingana na kichwa cha habari hapo
juu, tunajulishwa kwamba biandamu kama binadamu ni mtu wa wakati. Kuna wakati
ulikuwa mtoto, umekuwa mdada au mkaka sasa utakuwa mama au baba kesho na
utazidi kuendelea na wakati mwingine kadri Mungu atakavyokujalia.
Kipindi cha ujana ni kipindi chenye
mambo mengi mno, unakuwa na nguvu, mitazamo mbalimbali,ndoto nyingi za vitu
mbali mbali. Unakuwa pia fresh unakuwa pia na idea nyinginyingi ambazo
unaziwaza. Unakuwa unatamani kujaribu kila kitu unachoona kinakufaa. Unakuwa na
wigo mpana sana wakufanya na kutatua mambo mbalimbali.
Ukiwa kijana sio kwamba ndo mahali
pa kustarehe, sio mwisho wa basi. Bado safari inaendleea zaidi na zaidi.
Kwa hiki kipindi kinaweza kuwa kizuri
au kibaya kwako kama hutakitumia vizuri.Sasa kuna mambo ya kufanya ili
kumaximize mda wako wa ujana inabidi utambue mambo yafuatayo:
MAMBO
YAKUELEWA NA KUFANYA UWAPO KATIKA KIPINDI CHA UJANA.
1. Upo kwenye kipindi cha kuelewa
mda/Season of understanding the times
Unachotakiwa kufanya ni kumueka
Mungu wa kwanza, huwezi kumweka Mungu ukashindwa kitu. Huu ni mda wa wewe kama
kijana kukaa na Mungu vizuri ndiyo baadae yako itakapokuwa njema. Tunaambiwa
tuutafute kwanza ufalme wa mbinguni ndivyo na mengine yote tutakapozidishiwa.Kwa
hiyo ni vizuri ukaelewa hiki kipindi ni cha kumtanguliza Mungu kwa kila
jambo.
2.Ni mda wa ndoto na maono /Season
of dreams and Visions
Ni kipindi kila kijana anakuwa na
ndoto na maono mengi ambayo anatakani yaje yatimie baadae. Kama Yusufu
alivyoota ndoto yake ya kuja kutawala badae,haikutimia kesho yake ilichukua mda
na ilitaka uvumilìvu na utii kwa Mungu kwa hali ya juu sana. Tuwe na ndoto na
maono lakini pia tuwe na uvumilivu na utii wa Neno la Mungu ndivyo tutakavyofanikiwa.
3. Season of learning lessons/ Ni
mda wakujifunza
Elimu inatakiwa ikuandae kuja
kufanikiwa. Lakini pia wewe kama wewe unafanya nini kwa kutumia elimu unayopata
sehemu mbali mbali? Huu ndo mda wa kujifunza vitu vingi ambavyo baadae vitakuja
kutusaidia.Tusome vitabu tuudhurie training etc ambayo vitatujenga na kutupa
maarifa zaidi na zaidi.
5. Season of development/ Ni kipindi
cha maendeleo
Hapa ni kujiandaa na badae
yako/uzee. Huu ndo mda wakujijenga kiuchumi, kifamilia na kila kitu kikipita
kipindi cha ujana hakirudi. Ni vyema ukatumia vizuri ujana ili uweze kuendelea na
njia yakuendelea inaanzia kwa Mungu.
NJIA
KUU MBILI ZAKUKABILIANA NA KESHO YAKO
1. Expectation of rewards is the
result of preparation .Kama usipojiandaa leo usitegemee kupata mema uko
mbeleni.
2. Fear of repercussions is the
result of lack of preparation ,Kwahiyo ni vizuri tukajiandaa vyema.
Mahali pa kujiandaa
1. Spiritual Preparation/ maandalizi
ya rohoni
Tusome 1Yohana 2:14 Nadhani hamna
asiyeelewa jinsi ya kujiandaa kiroho
2. Mental preparation/kujiandaa kiakili.Tafuta
maarifa mbali mbali yatakayokupa kujifunza mambo yatakayopanua akili yako na
kukupa maarifa mbali mbali. Jiandae kiakili kwamba hapa kwenye ujana sio mwisho
wa maisha,utapita na stage nyingine itakuja. Kwa hiyo ni vyema tukawa tayari
kiakili
3. Physical Preparation/ maandalzii
ya kimwili
Fanya mazoezi ili kumaintain mwili
wako. Ishi vizuri sawasawa na maagizo Mungu aliyoagiza tuyaishi.
5. Social preparation/ maandalizi ya
kijamii
Hapa ni vizuri uka socilize na watu
mbali mbali, ndo kipindi chako cha kujamiiana na watu mbali mbali.Lakini pia
maarifa yanaitajika ili kujua namna gani ya kurelate na watu unaoitaract nao.
YOTE YA YOTE UKUMBUKE TU HUWEZI KUWA
KIJANA MARA MBILI. KIPINDI CHA UJANA NI ZAWADI TOKA KWA MUNGU. TUUTUMIE UJANA
VIZURI KWA HEKIMA NA MAARIFA TULIYOPEWA NA MUNGU.
IMETAFSIRIWA NA DADA DOROSELA KIMARO
No comments