YOUNG LEADERS AND BOOKS / VIONGOZI VIJANA NA USOMAJI WA VITABU
YOUNG LEADERS AND BOOKS / VIONGOZI
VIJANA NA USOMAJI WA VITABU
Viongozi ni wasomaji wa vitabu?
Kuna msemo unaosema sio kila
wasomaji wote wa vitabu ni viongozi, lakini kila viongozi ni wasomaji. Not all readers are leaders but all leaders must be readers.
Kusoma vitabu inakuboresha kujua
lugha na maendeleo kwa maisha ya kibinadamu.
Kadri unavyosoma vitabu ndivyo
unavyojua au kufahamu mambo mengi, na kadri unavyojua ndivyo unavyowezapata
matokeo.
Katka vitabu unaelimika na kuwa
muelewa,unajua umuhimu wa mafanikio ktk maisha. Hosea 4:6 Watu wangu
wanaangamizwa kwa kukosa maarifa....
Usipokuwa msomaji hupati maarifa
usipopata maarifa unaangamizwa na wenye hila. Kama mpendwa husomi Neno ili
upate maarifa atakuja mtu na mstari wake atakuyumbisha tu...hutakuwa na nguzo
ya kusimamia
TUONE WASOMI 3 WA KWENYE BIBLIA
1.DANIEL
......mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu,
nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii, ya
kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.Daniel 9:2
Kwa kusoma vitabu aliweza kugundua
hili neno la Bwana
2. YESU KRISTO
17 Akapewa chuo cha nabii Isaya,
akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
18 Roho wa Bwana yu juu yangu,Kwa
maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.Amenituma kuwatangazia
wafungwa kufunguliwa kwao,Na vipofu kupata kuona tena,Kuwaacha huru waliosetwa,
19 Na kutangaza mwaka wa Bwana
uliokubaliwa. Luka 4:17-19
3.MTUME PAUL
Ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa
vile vya ngozi. 2 Tim 4:13
Mtume Paul anaagizia aletewe vitabu
ili asome, inaonyesha yeye ndie wa kwanza kuwa na Maktaba ya vitabu.
Anza leo kuweka maktaba ya vitabu
nyumbani mwako,nunua vitabu,usome vitabu
Bill Gates na rafki yake Paul Allen kwa kusoma
Magazeti waliweza kugundua na kuanzisha Computer project.
Miongoni mwa watu waliofanikiwa
sanasana viongozi ni wasomaji wazuri wa vitabu. Kuna baadhi ya misemo inayoweza
kutusaidia;
a) Kitabu ni zawadi unayoweza
kufungua tena na tena.
Garrison Keillor
b) Uelewa ni daraja katika matatizo na
matumaini. (Uelewa tunaupata kwa kusoma)
Kofi Annan
c) Kitabu kinachomletea mtoto tabia
ya kusoma ni kizuri kwake.
Maya Angelou
d)Kusoma itolewe kama zawadi kwa
mtoto na sio kwa lazima au kazi.
Kate DiCamillo
e) Kusoma ni mazoezi ya akili.
Richard Steele
Kwa kusoma unapata faida nyingi.....Kujua
historia
Mathayo 12:3
Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda
Daudi, alipokuwa na njaa,yeye na wenziwe?
Hawa watu wangekuwa wamesoma
wasingemnung'ukia Yesu kuwa wanafunzi wako wanavunja na kula siku ya sabato
1 Tim 4:13 Ufanye bidii katika
kusoma na kuonya na kufundisha.
Nami nakusihi leo ufanye bidii ktk
kusoma,utajua ahadi za Mungu,utasimamia imani yako,utaweka tumaini la kweli katika
Kristo.
Imeandaliwa Dada Furaha Mosha na kuwekwa hapa na Magreth Gift Mushi
No comments