KEY TO ACADEMIC SUCCESS/ FUNGUO ZA KUKUSAIDIA KUFAULU MITIHANI
KEY TO ACADEMIC SUCCESS/ FUNGUO ZA
KUKUSAIDIA KUFAULU MITIHANI
Mungu anapenda sisi tupate maarifa.
Na maarifa haya tunayapata kwa namna mbalimbali na moja wapo ni kwa kwenda
shuleni. Tunapokwenda shuleni tunaenda kupata maarifa mapya na kuongeza
ufahamu.
Isaya 11:2[2]Na roho ya BWANA atakaa
juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa
na ya kumcha BWANA;
Roho hizi 07 za Mungu zinakaa ndani
mwetu. Kama zilivyotabiriwa kuwa juu ya Yesu Kristo. Tunapaswa kuwa na bidii
katika kutafuta maarifa na siku tutakayoacha kutafuta maarifa ni siku tunaingia
kaburini. Tuko hapa pia kupata maarifa.
: FUNGUO 05 KWA UFAULU MZURI
1. MALENGO /FOCUS
Kuna mambo mengi sana
yanayotushawishi sisi kama vijana. Na yanaweza kutuvuta sisi tuyape Muda wetu.
Na kama mwanafunzi hauwezi kufaulu mitihani yako kwa kuwa katika mazingira
yanayokusumbua na kukuangaisha. Wanafunzi wengi wanaenda shuleni na akili
zao hazipo shuleni.
Huwa unapata matokeo mazuri kwa kile
ulicholipia gharama kubwa. Kuna kanuni ya Pareto inasema 20% ya kile unachofanya
inakupa 80% ya matokeo. Unapaswa Kujua kwa 20% na kuweka MALENGO yako hapo
2. DETERMINATION/KUAMUA
Unapaswa kuamua. Kuna vitu vingi
unaweza kuvifanya kuwa visingizio vyako. Ila tunapaswa kuvuka visingizio vyetu.
Tumekuwa watu wa kusingizia mifumo na wazazi wetu. Wisingizio sio suluhisho.
Unapaswa kukiacha visingizio na kuchukua hatua.
3. KUWA NA BIDII/ HARD WORK.
Mbele ya kila mafanikio kuna sura ya
kufanya kazi kwa bidii. Hakuna kitu kinatokeaga kama hakuna mtu aliyefanya kazi
kwa bidii. Vitu havitokei tuu kwa sababu tunakiri na kuvitamka tuu ila
vinatokea kwa sababu pia ya kufanya kazi kwa bidii kukiri na kuamini pekee
haitoshi. "There is no a substitute of hard work "
Hakuna kitu kinatokea kama kama
hakuna mtu atakayekifanya. Hata kwa wanafunzi hauwezi kufaulu mitihani
kwa kuamini kwamba utafaulu tuu. Ila ni lazima usome kwa bidii.
4. KUSOMA/ STUDYING
Danieli 9:2[2]katika mwaka wa kwanza
wa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya
miaka,
Kuna nguvu katika kusoma vitabu.
Kuna utajiri mwingi sana umefichwa kwenye vitabu. Tunapaswa kusoma vitabu
kupata majibu ya maswali mengi tunayokuwa tunajiulizaga.Hii point nitakuja
kuielezea zaidi Katika somo la Nguvu iliyoko katika kusoma vitabu ambayo nitatuma hapa katika somo lijalo.
5. KUMWAMINI MUNGU.
Hauwezi kufanikiwa bila msaada wa
Mungu unamwitaji Mungu kila wakati katika maisha yako ya masomo kama mwanafunzi
uwako shuleni. Mtangulize Mungu katika kila jambo unalotamani kumwona Mungu
amakutangulia.
Imeandaliwa na Mwl. Magreth Gift Mushi Mawasiliano 0654 444433
No comments