Highlights

A YOUTH THAT GOD USES / KIJANA AMBAYE MUNGU HUMTUMIA.


KIJANA AMBAYE MUNGU ANATAKA KUMTUMIA/ THE YOUTH GOD USES

Mungu anapenda vijana na anatamani kuwatumia kwa sababu KIJANA akifanya vizuri atanufaika na huo ubora na pia marafiki zake watanufaika na huo uzuri, pia ndugu zake watanufaika. Na vile vile KIJANA akiharibika kwanza atajiaribu mwenyewe, atawaharibu na ndugu zake pia kwa namna moja au nyingine. 

Kama KIJANA umeokolewa ili Uwe useful au wa maana kwa jamii, kanisa, taifa na sio kuwa chochote yaani useless.Unapaswa kuacha na kuweka alama katika ulimwengu huu.Hata familia yako wanapaswa wajisikie furaha kuwa na Wewe na kumshukuru Mungu kwamba ulizaliwa, sio ikitokea upo nyumbani kila mmoja anatamani siku ziishe uondoke urudi shule au kazini. Kwa sababu hawaoni unaongeza nini kwao. You should be a contributor and not a consumer. Hata unapokuwa nyumbani kwenu haihitaji nguvu nyingi kukufanya watamani kuzidi kuwa na Wewe na wakumiss unapokuwa haupo. Ni kwa kufanya vitu vidogo tuu. Hakikisha nyumba ni safi umedeki, osha vyombo n.k sio kila dakika uko na simu yako unanyoosha vidole tuu Hata nguo hautaki kufua. Lazima watamani uondoke mapema kwa sababu Wewe ni mzigo kwao

Kuna huu usemi au imani potofu ipo kwa baadhi ya vijana kwamba Mungu anawatumia tuu wale watumishi waliopakwa mafuta kuwa madhabahuni ambao ni watu wazima. Ambao wanahubiri injili ya Kristo, Mungu hapigwi au hawekewi mpaka na umri au mwonekano wa nje wa mtu. Anaweza kumtumia mtu yeyote yule haijalishi ana au hana Hadhi yoyote katika jamii au Hata jinsia ya mtu haijalishi mbele za Mungu. 

Bado Mungu anawahitaji watu wa Marika yote katika kazi ya kuukuza ufalme wake. Hivyo kigezo cha Wewe kuwa KIJANA hakikuzuii kumtumikia Mungu kwa sababu Mungu anakuhitaji sana umtumikie ungali bado KIJANA kwa ajili ya kuukuza ufalme wake. Mungu anataka kufanya kazi na Wewe ungali bado ni KIJANA kwa sababu una nguvu na neno la Mungu limekaa ndani mwako

1 Yohana 2:14 [14]…. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

MAMBO 05 YAFUATAYO YATAKUSAIDIA UWE KIJANA AMBAYE MUNGU HUMTUMIA.

 1. USHIRIKA
Yesu alisema Mathayo 18:20 [20]Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
Ushirika ni kiungo muhimu sana kwa waamini kwa ajili ya kuunganishwa na Roho Mtakatifu. Mungu amekusudia sisi tuunganishwe pamoja kwa ushirika wa Roho Mtakatifu. Ndio maana huwa tunasema Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba na Ushirikia wa Roho Mtakatifu.....

 2. KULIPOKEA NA KULIISHI NENO
Kulipokea na kuliishi neno la Mungu ni ni namna bora na ya haraka sana ya Wewe kukua. Hauwezi kukua kiroho kama sio msomaji wa maneno yake. Kukua kwako katika Yesu ni matokeo ya upendo wako kwenye neno la Mungu. Na namna unavyolitumia katika maisha yako ya kila siku

 3. KUTII
Kukua katika kristo kunahitaji jitihada sana. Na hii ndio njia unayoweza kumfurahisha Mungu. Hauwezi kuwa na manufaaa kwa Mungu kama haukui katika neno lake na katika Yesu kristo. Kukua katika Kristo ni kwa kutii neno la Mungu. Ukuu uliopo katika ufalme wa Mungu ni kwa kutii.  Zaburi 119:9 [9]Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.

 4. BIDII
Kukua ndani ya Kristo kunahitaji jitihada. Sio kitu kinachokuja tuu bila kujua. Karibu kila kitu katika dunia yetu hii kinatufundisha kuwa tunahitaji kuwa na bidii. Na kwa Mungu pia bidii inahitajika

 5.KUTUBU
Huwa tunaanguka dhambini kila Mara. Huenda ni kwa sababu ya uchanga kiroho lakini haimaanishi kila siku utazidi kuwa mchanga kiroho. Unapaswa kuwa na tabia ya kumwomba Bwana Yesu akusamehe pale unaposea kwa sababu sisi ni wakosaji. Na Mungu hawezi kukutumia kwa viwango anavyovitaka yeye kama tutazidi kuwa wachafu kiroho.

Ninapohitimisha napenda kusema kuwa

1. Mungu anachukia dhambi. 
Kila unapokuwa unakwenda weka hili akilini mwako, kwamba Mungu anachukia Dhambi na Wewe kama mtoto wake unapaswa pia kuchukia dhambi kama Baba yako. Dhambi inaweza kukufanya uonekane sio chochote au lolote.

2.Hauwezi kuishinda dhambi kwa nguvu zako za kimwili. Will power.  unahitaji sana msaada wa Mungu kuweza kushinda dhambi na madhara yake. Mwite Yesu akuvushe katika nyakati unazoona unakaribia kuanguka dhambini au unapokuwa umemtenda Mungu dhambi

3. Kuwa makini na kutokuchaguliwa /disqualification.
Utakapoendelea kuishi maisha ya dhambi na Yesu akija Leo uhakika wa kuondoka nae hauna kwa sababu ya dhambi. Unapaswa Kujua majukumu yako na kuyafanyia kazi na kujiwekea nidhamu binafsi. 
1 Wakorintho 9:27 [27]bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Ili Uwe KIJANA AMBAYE MUNGU humtumia unapaswa kumpa Yesu Kristo maisha yako. Na kama ulikuwa umerudi nyuma unayo nafasi sasa ya kutengeneza na Yesu tena Yohana 1:12-13 [12]Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; [13]waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

imeandaliwa na Mwalimu Magreth Gift Mushi.Kwa mawasiliano zaidi magrethgifth@gmail.com

No comments