Highlights

TAFSIRI YA KISWAHILI YA KITABU CHA KUTUNZA UTAKATIFU KATIKA MAHUSIANO


TAFSIRI YA KISWAHILI YA KITABU CHA KUTUNZA UTAKATIFU KATIKA MAHUSIANO PRESERVING PURITY IN RELATIONSHIP KILICHOANDIKWA NA MWANDISHI JOHN E BALOGUN


Kwanza tuelewe mahusiano haina maana ndiyo mmeshakuwa mme na mke,Ni mpaka kiapo kifanyike mbele ya madhabahu ndo hapo utakuwa mke na mume, hivyo tunanapaswa kufanya yafuatayo ili mahusiano yetu yadumu katika utakaso, yani usafi na yakumtukuza Mungu  sababu mahusiano mengi yanaishia kuharakisha kufanya tendo la ndoa kitu ambacho vijana wengi wanafanya:

kuomba msaada au kuondoka kwenye mazingira ya kukupelekea kufanya tendo la ndoa endapo umeshikwa na hali hyo. 

    Warumi 5:19-20

[19]Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.[20]Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;



Unapoomba msaada endapo mmoja wenu kwenye uhusiano akajikuta katika hali ya kutaka kufanya tendo la ndoa, omba kwa watu sahihi ambao wanaweza kukushauri ushauri sahihi

Wagalatia 6:1-2

[1]Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.

[2]Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.



Mkristo (mvulana/msichana) anaweza kuanguka kwenye dhambi ya kuzini kwa uzembe wake mwenyewe, kwa hiyo hapa kila mmja aweke hali ya kushinda jaribu hilo lakini mmoja wapo akilega basi mahusiano yenu yanapoteza ile hali ya utakaso /usafi ndani yenu.

1 Wakorintho 10:13

[13]Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Tunza mahusiano ya ukaribu na roho mtakatifu 

 Roho mtakatifu yu ndani mwetu siku zote basi katika mahusianoo tunapaswa kuwa karibu nae sana maana tunafahamu kazi za Roho Mtakatifu akiwa ndani mwetu. 

Wakolosai 2:5-7

[5]Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.[6]Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye;[7]wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani.



USIFANYE MAHUSIANO YA SIRI. 

Kwa watu tunaoishi maisha ya wokovu inatupasa kuwa na mahusiano ambayo sio ya siri na sio tu wenye Malengo ya kuoana hata wengine ni marafiki wa kawaida na ni jinsia tofauti ni lazima kuwa wazi  ili kuepuka yale mabaya ambayo mnaweza shawishika.

Kwa mahusiano ya kiuchumba ni vyema kushirikisha watu mnaoamini watawasaidia kutimiza lile Kusudi la ukuutunza usafi wa moyo wawasaidie kuomba na kuwashauri nini cha kufanya kukaa mbali na kuikimbia zinaa. Mapenzi ya siri ni kujijengea maumivu na msiba usiopoa

    Hapa ina maana upo kwenye mahusiano lakini nyumbani hata marafiki zako hakuna anayejua hata wakubwa wako na hata walezi wako wa kiroho hawajui, hii siyo nzuri, na wanachuo wengi wao wanahisi kwamba watakuja kujua baadaye hivyo wanafanya siri. Aisee usije ingia kwenye mahusiano ya aina hii kwa sababu hii inaonesha malengo mbele, kama malengo yapo kwanini kujificha? Faida za uhusiano uliowazi ni kuwa unao uwezo wa kuomba msaada wa maombi kwa watumishi kuhusu uhusiano wenu. Mahusiano ya siri yanauwezo mkubwa wa kukuangusha dhambini

Waefeso 5:11 Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;



Wasiliana na mtarajiwa wako ni nani wa kuomba msaada endapo ikatokea amekiuka maadili ya uchumba, haipaswi mkristo kuishi kwa kuficha dhambi. 

Waebrania 13:17

[17]Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi...

Ikatokea mtarajiwa wako hana hata mtu wa kukusaidia akionesha khali hiyo basi sivyo yani hata baba wa kiroho basi ogopa kujiingiza kwenye mahusiano hayo.



     KUWA MTU WA TOBA

Hakuna kitu kizuri katika maisha ya mwanadamu kama kujua umekosea na ukaenda mbele za Mungu kutubu.Yesu yupo anaokoa, anasamehe yote na anatupa rehema ya msamaha wa dhambi. Inapotokea umeanguka katika uzinzi na mpenzi wako kwanza mjue mmekoseana maana mmetoka katika kusudi na zaidi mmemkosea Mungu hivyo inatakiwa kukiri na kutubu ndipo Mungu atawarejeshea Moyo safi na roho iliyotulia ndani mwenu Zab 51:10-12 na furaha ya wokovu itarejea.                                                                                                                                                  

1 Yohana 2:1-2

[1]Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, [2]naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa ulimwengu wote



Ø  Wewe na mwenzi wako mnatakiwa kuwa na watu muhimu mtakaowategemea katika taarifa zenu za mahusiano.Watu wa kwenda kuwa wanaweza kuwa watu wakiroho ama watu ambao mliwahusisha uwepo wa mahusiano yenu na hivyo mnakuwa mnaweza kwenda muda wowote kuwapa taarifa ya jinsi mahusaino yenu yanavyokwenda au jambo lolote kuhusu mahusiano yenu .



Omba msaada

Yamkini wewe na mpenzi wako mmejijengea tabia ya kutembeleana kwenye nyumba zenu ambazo hazina wazazi wala marafiki ambao watawafanya msiingie dhambini na ikatokea mmoja ana uhitaji au tamanio la kimwili wewe ambae uko vizuri tafuta msaada kwa mtu ambae ni sahihi na ana uwezo ya kumhimili mwenzio kwa upole bila kusababisha baya lolote na kwa imani Mungu ataweka sawa yote .



Jambo lingine usiwe kwenye mahusiano wewe kama binti mkristo na mtu ambaye ni mpagani asiyemjua Mungu kwa majina mengine yatima wa kiroho. Kwani utapata shida maana anakuwa hajui anachokiamini.Hapo ndiyo ule mstari wa biblia unatumika "usifungiwe nira na wasioamini



Ø  Kupata mchumba sio swala la kiroho tu. Inabidi mdada uonekane ili mkaka aje akuchumbie.Sio kukaa tu ndani au kila mtu anaekuja wewe hupati hata muda wa kuwasikiliza



Ø  Kabla ya kuwajulisha wazazi na walezi kanisani muwe mmeshachunguzana. Hii sio kuficha mahusiano ila kwa sasa ni muhimu maana kuna watu ni wakristo ndio lakini kuna vitu hawaviamini mf matambiko, kujamiiana n.k. sasa mmekutana leo kisa ni mwanakwaya ukaamua kumpeleka kwenu. Kesho anakwambia anataka mfanye mapenzi kwanza na mengineyo



Ø  Kuwa na uwezo wa kujitegemea. Mimi hapa naona si kwa wanaume tu hata wadada. Ukisoma mithali 31 utaelewa. Basi sawa hela huna hata kazi za nyumbani huziwezi na unataka ndoa??



Ø   Kuondoka kwenu. Kuna watu hadi mama zao waruhusu vitu ndo maana wao wafanye. Mungu atusaidie, kuna changamoto  sana hapa.



Hivyo basi wewe kama wewe unahusika moja kwa moja katika kutengeneza ndoa yenye furaha na amani na ndoa utakayo ifurahia. Hii ni  kwa sababu ndoa iliwekwa na Mungu ili wawili hawa waifurahie lakini shetani amewateka watu akili wanashindwa kuziandaa ndoa ambazo Mungu anataka  tuwe nazo. (Dada usikubali shetani akufanyie hivyo)

Utataengeneza vipi hiyo ndoa ni kwa kufuata siri hii hapa .



Unapomtafuta mtu ambaye ndie utayeishi nae maisha yako yote  ya hapa duniani mpaka utakapo kufa unapaswa uwe makini sana  na usilete mchezo na  hilo swala aiseee.

Hakikisha huyo mtu anamjua Mungu sana  na ana hofu ya Mungu hii itafanya ndoa yenu iwe na amani na furaha kwasababu ninyi wote mna hofu ya Mungu.  Sasa wewe endelea  kuruka ruka huko, humtafuti Mungu huna hofu ya Mungu alafu utegemee kumpata mtu aliyetulia na mwenye hofu ya Mungu, hapo unasubiri sana na Mungu atakupa wa kufanana na wewe.



Hatua ya pili  ni ya  Mwanaume kumuomba ukubali uwe mke wake, hapo kazi kwako kukubali au kukataa,  na kama naona huyu mtu hana muelekeo kwa  namna Roho mtakatifu anavyokuongoza ni bora ukakataa na kumuambia Mungu najua Kwenye ghala yako Mungu wanaume hawajaisha naomba unipe wa kufanana na mimi, Mungu wangu na Mungu atakupa



 Kama kwenye hatua ya pili ulisema "ndiyo" na ukakubali kuwa mke kwakwe pengine mkaweka na alama kwa maana pete ya uchumba basi hatua inayofuata ni kuanzia kumsoma zaidi tabia na mwenendo wake na hapa hata watu na wazazi wanakuwa wanafahamu mahusiano yenu maana yamekuwa sio siri tena., Ila hupaswii kubweteka na kujiona tayari umesha kuwa mke, wakati bado uko kwenye hatua tu.

Hapa shetani nae huwa makini sana  na anaweza kuinua vita ili tu msitimize kusudi la Mungu maana najua mkishaoana yeye anaaibika. Lakini pia ukigundua kuna vitu huyo mchumba anavyo Na siyo kusudi la Mungu, basi ingia magotini na mlilie Mungu akupe macho sawa sawa.



Lakini hatua nyingne ni kuhakikisha kila mtu baina yenu ninyi wawili mnakuwa mnalindana, kwa maombi, nidhamu na kurekebishana mnapoona mambo hayaendi sawa ili kutengeneza siri nyingne hii hapa chini.



Kutengeneza malengo yenu yambele, kama mlikuwa wazi kipindi cha uchumba, kuambia ukweli, kuishi maisha halisi na si ya kuigiza, kushirikishana kila kitu, kuambiana matatizo na kuwa na kutafuta suruhu kwa pamoja, kupanga mipango yenu ya baadae kwa pamoja, kwa kifupi kumfanya mwenzio awe ndio rafiki yako wa karibu wako,  kwa kufanya hivyo mtakuwa mmejenga malengo mazuri ya mbele  na mtafurahia maisha yenu ya ndoa. KITABU HIKI KIMEFANYIWA UFUPISHO NA

 MWANDISHI MAGRETH GIFTH MUSHI PAMOJA NA MABINTI WA HUDUMA YA

 A LADY WITH A PURPOSE.

 KWA MAWASILIANO ZAIDI

255 654 444433


@ June 2019


Download hapa

No comments