UFUPISHO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA KATIKA KITABU CHA BIBLE SENSE OF GETTING INTO MARRIAGE
UFUPISHO KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA
KATIKA KITABU CHA BIBLE SENSE OF GETTING INTO MARRIAGE {KUINGIA KWENYE NDOA KWA
MTIZAMO WA KIBIBLIA}.KILICHOANDIKWA NA DAVID OYEDEPO.
Kitabu kinaelezea jinsi au namna ya
kufanya ili ndoa yako iwe yenye furaha na amani. Ndoa imeanzishwa na Mungu
ili kuwafuraisha wanadamu. Ndoa ni kitu kizuri kinachounganisha watu pamoja,
nikimaanisha kwamba mume anapoungana na mke pamoja katika kujenga familia
tunaona kwamba undugu unakua zaidi.
Kwa hiyo ili uwe na ndoa njema ni
lazima ndoa yako misingi yake ianzie kwa Mungu,ili ndoa iwe ndoa lazima MUNGU
asimame katikati tukijua kwamba yeye ndie mpaji wa vipaji vyote, yasiwe ni
mawazo yako tuu au hisia ukahitimisha kuwa huyu ndiye, mambo yakiwa
mabaya hata Mungu hatakusikiliza maana hukufata anavyotaka Yeye. Nanukuu kutoka
sehemu katika kitabu hiki imeandikwa kwamba
“Marriage is a good thing established by God,
for the benefit of man. But to enjoy the benefits, it must be entered into as
God intended it to be”.
(Ndoa ni kitu kizuri kilichoanzishwa na Mungu,
kwa manufaa ya mwanadamu. Lakini ili kufaidi manufaa, lazima ufanye kama Mungu
alivyopanga). Hivyo ndoa ni kitu kizuri Mungu akisimamia.
Kutengeneza ndoa njema huanza na wewe
mwenyewe ukikubaliana na changamoto zote na kujua jinsi ya kuzitatua ili
kupiga hatua mbele zaidi, kuna msemo unajulikana sana kwamba “Usikosee
kuoa/kuolewa” Je, walikua na maana gani kusema hivyo ..ni wazi kuwa walijua
changamoto zitokanazo na hilo.
Pia unapotafuta mwenzi haitokei tu
ulalapo au uotapo ndotoni ni akili yako inayokuongoza na kukuwezesha kutambua
nani atakayekufaa kuliendesha gurudumu la maisha yenu, hivyo ndoa ni kitu
kizuri ambacho MUNGU akiwa ndani mwake hudumu daima.
»Kabla ya ndoa lazima mchunguzane ili
kila mmoja amjue mwenzie vema, sio mnakutana siku moja mkapendana wiki mkataka
ndoa ikafungwa...aisee matatizo yakitokea nani alaumiwe?? hapo ndipo utaona
kila moja anamlaumu mwenzie na kujiona yeye ni mwema asie na kosa hata kama
yeye ndo mwenye makosa.
Kumtafuta mwenzio
- Lazima awe mwamini. Hakuna makutano kati ya mwenye dhambi na mcha Mungu. KUMBUKA: ni rahisi sana mwenye dhambi kumshawishi mcha Mungu kutenda dhambi, kuliko mcha Mungu kumgeuza mwenyewe dhambi.
- Hapa unatakiwa uwe makini Weka vigezo vyako, kuwa makini na mtu unayeingia katika mahusiano naye. Sio rohoni tu au kimawazo. Na amesema vizuri kabisa usianze kuang'ang'ana na mtu asiyeamini maana ni rahisi sana wewe kurudi nyuma kuliko kuendelea mbele. Hata kama ni nzuri kiasi gani au unatamani iwe ndo hiyo hiyo kama sio mwamini ni bora ukaacha ili ufate mapenzi ya Mungu. Ametolea mfano wa agano Mungu aliloingia na Abrahamu kwamba wasioe nje ya ukoo wao.Pia sisi tumesisitizwa sana kutokuangalia au kutafuta wale wasio njia moja na wewe. Ni bora uue mapenzi yako kuliko uyafate baadae mambo yashindikane. Hata Mungu hatakusikiliza maana Yeye pia analiangalia neno lake apate kulitimiza.
»UCHUMBA
Mara nyingi kwa kipindi hiki watu
wengi hatufuatilii hii hatua, tunakurupuka halafu tunakuja kujutia
baadae. Ni lazima kuwa katika uchumba kwa muda ili tuweze kuchunguzana na kujua
tabia zetu kiundani zaidi, ili kama mtu hajapendezwa na mambo anayoyafanya
mwingine, tuweze kurekebishana, kabla hatunaingia kwenye ndoa. Uchumba
unasaidia sana watu wanajuana vizuri.Hiki ni kipindi cha kuchunguzana sasa ili
kuimarisha uhusiano wenu, je mnaendana, tabia zenu zikoje (unapenda nini,
upendi nini, unafuraishwa au hufuraishwi na nini, unapendezwa, hupendezwi na
nini n.k) Kupitia hayo unaweza tambua anakufaa/ hakufai.
»Maombi pia hubadilisha usichoke
kuomba omba kwa Imani nawe utapokea kwa imani
»MITHALI 18:22 Apataye mke apata kitu
chema; naye ajipatia kibali kwa BWANA.
Alpha ana nyimbo inaitwa
Yes...kuna verse inasema “he who finds a wife finds a good thing, give me
wisdom to protect this love…(Yeye apataye mke, apata kitu chema, nipe hekima ya
kulinda penzi hili) ni kweli kabisa kwamba apataye mke apata kitu chema.
»Ndoa si kwa ajili
ya wavulana na wasichana ni kwa ajili ya wanaume na wanawake tena waliojiandaa
vema.
»Ndoa ni chaguo na si
kulazimishwa/kutumia nguvu. Ili ndoa iwe ndoa lazima kuwe na makubaliano baina
ya watu wawili wenye msimamo mmoja wa kuanza maisha yao mapya kwa pamoja vilevile
mkiishi maisha yenu kama nyie, msiruhusu kuishi maisha ya kuangalia wengine
wanaishije mtafeli. Tunapoona ndoa nyingi zinafeli kwa sababu hiyo ya kuangalia
akina fulani wanaishije, daima usiishi maisha ya kuangalia akina fulani
wanaishije,wanakula nini, wanavaaje...ishi maisha yenu nanyi mtabarikiwa
haijalishi ni maisha gani mliyonayo, daima penda kujua njia za kukupandisha
viwango kutoka ulipo kuelekea juu zaidi ya ulipo hiyo ndio njia sahihi kuliko
kutafuta mbinu za kupindua wengine.
- Ndoa inajengwa na mume na mke wenye kutambua wajibu wao kama ilivyo agizo la Mungu mwenyewe, mume kumpenda mke na mke kumtii mume, Waefeso 5:24-25
Ndoa inajengwa na watu wenye muelekeo
unaofanana, compatibility Ndoa lazima iwe ni ya makubaliano, Ndoa ni
chaguzi na sio shuruti, kila mtu ana haki ya kuamua. Kipindi cha uchumba ndio
kipindi cha kujua mbivu na mbichi, yaani ni kipindi cha kutafuta ukweli
kwa sababu uchumba unavunjika na sio ndoa na ni kipindi pia cha kuaminisha
upendo wako kwa mwenza wako, pia na kubakia ni ya watu wawili, wazazi au
marafiki huwa wanafuata baadae. Katika wakati huu, una haki ya kukataa, kukemea
kuhoji na sababu, tabia vitu ambavyo huviamini na ambavyo havikusaidii na kumpa
Mungu utukufu.
Makubaliano
Baada ya kumpata ambaye unaona analingana na
viwango vyako ni lazima pia mkubaliane. Hauwezi kuongozana tu kama
hamjakubaliana. Ni lazima akubaliane na viwango ulivyonavyo.Na hutakiwi kuogopa
kuonyesha msimamo wako. Weka wazi unachotaka kama akikubalina anaweza utajua
kama ndo yeye au sio. Nimesoma na kitabu cha Mwalimu Mwakasege cha kabla
ya kuolewa anasema uwe wazi kabla hamjaenda kwenye hatua nyingine. Usipoteze
muda kuremba remba mtu au kuficha kusema nini unataka, hata kama ni namna ya
kuchana nywele ni lazima wote mkubaliane.
Kuchunguzana kwa pande zote mbili.
Lazima umchunguze mwenzio vizuri sana
ili kujua kila kitu kabla ya kuingia kwenye ndoa. Na haitakiwi kuwa miezi tuu
au muda mfupi sana. Mnatakiwa mjuane vizuri ili mkiingia kwenye ndoa kusiwe na
tofauti. Mwandishi amesema ndoa nyingi zina shida kwa sababu hapa wengi wanaona
madhaifu lakini hawasemi wanajipa moyo au kuendelea. Na pia hutakiwi kusikiliza
ndugu, marafiki n.k ni wewe utaishi naye uko ndani usiku na mchana
kwahiyo ni vizuri ukafanya uchunguzi uridhike wewe sio ndugu au
yeyote. Kama hujaridhika na mtu ni bora umwambie tu ukweli. Katika
hali iliyo tulivu si kwa kumtumia ujumbe wala kumpigia simu, ni kukaa ana
kwa ana na kuambiana tu ukweli. Kabla ya kukurupuka na kuenda
kutambulisha kwa wazazi, ndugu utajikuta tu wewe ni wa kutambulisha /kutambulishwa
kila mara na familia pia itakuchoka.
Muendelezo
Kuendelea ni hatua nyingine ambayo
baada ya kufahamiana ukaona tabia, madhaifu yenu mnaweza kuchukuliana basi ni
jambo la ndugu familia na wazazi kujua pia lakini kipindi hiki yaani unakutana
na mtu siku mbili wazazi hawamjua ila WhatsApp wako wote wamesha mjua sio kwa
kurusha huko. Ukiwa hivyo utaonyesha wangapi maana hamkuja mtaachana tuwe
makini. Kama vingine uko juu viko sawa ndo uendelee na hapa. Kama haviko sawa
usiendelee maana matatizo yatakayokupata wewe ndiyo utakayehangaika maana
maamuzi uliyafanya wewe. Ni lazima uwe makini.
Kulindana
Hiki bado ni kipindi cha uchumba kwa hiyo
ni vizuri mkalindana kwa kuombeana ili msije mkaanguka dhambini. Ni lazima
uweze kujichunga ili usimsababishie mwenzio kuanguka pia. Hasa kwa wanawake,
sisi hapa ndio wa kuwasaidia wanaume maana sisi ndio tunayachochea zaidi mpaka
unakuta watu wanaanguka kwenye uzinzi. Ni vizuri tuweze kujizuia na kujitunza.Utakavyomsaidia
mwenzio ndivyo mtakavyoeweza kulifikia lengo salama.
Kukataa
Hapa ni kukataa tabia unazoona
zitakuja kuleta shida uko mbeleni. Hata kama vimetoka kwa ndugu ni lazima ukatae
na kuweka vigezo ambavyo huko mbeleni hazitaleta shida kwenye ndoa yenu. Ni
bora kurekebishana hapa kuliko kuja kuleta ugomvi huko baadae. Hii ni
hatua ya kuangalia mambo gani ambayo yanaweza kuharibu ndoa yenu msipokuwa
makini. Ndoa ni watu wawili na sio jamii nzima inayokuzunguka msije mkaruhusu
wengine kufanya shauri kwenye ndoa yenu. Hata kama ni wazazi mkaona kwamba hapa
mnamkosea Mungu ni bora na iyo ndoa isiwepo kabisa maana makabila mengine wana
mila ambazo kiukweli hazivumiliki kuliko umkosee Mungu ikose hiyo ndoa.
Jiandae kwa ajili ya wakati ujao.
Andaeni mazingira mnayoyaendea baada
ya ndoa, makazi malazi, sio mabinti tunategemea kuolewa na mwanume si ana pesa,
mie sihitaji kufanya lolote hapana hata binti nawe tengeneza mazingira yako
kama mke na mama mtarajiwa sio hata kupika mboga unaanza mpigia mama yako
utapika nin,i hapana nasi tujiweke tayari kuna mambo inabidi tujifunze kabisa. Hapa
ni tusikurupuke kufanya vitu. Ni lazima ujipange na kujiandaa vyema maana
mnaenda kuanza familia. Mahitaji yataongezeka. Ratiba zako hazitakuwa tena kama
za sasa hivi.
Kama kila kitu kipo sawa kuanzia hatua
ya kwanza ndio uendelee kufunga kabisa pingu za maisha.Kama hapana, kumbuka
uchumba unavunjika. Usilazimishe vitu vitokee. Acha mapenzi ya Mungu
yatimizwe.
Utambulisho
Mkiwa mmeridhika na
mmeshajuana, utambulisho ufuate, ili iweze kuwa rasmi baada ya hapo
sasa mnaweza mkachukua hatua ya kwenda
mbele ya altare. Kuweka nadhiri zenu mbele za Mungu na familia ikiwa mashahidi
kuwa sasa mke na mume rasmi.
NB:
Kuna mambo ambayo mkiyafanya wakati wa
uchumba mkiyapeleka kwenye ndoa lazima ndoa itayumba napo tuweni makini sana
tuweni na mipaka.
Mungu awabariki sana na Roho Mtakatitu
atuongoze kupata Mume mwema katika maisha yetu aliye sahihi kwetu.
NYONGEZA:
Kuna mambo 5 unayopaswa kuyafanya ili
uwe na kujipenda na kujiamini:
1. Kubali nini au nini kilikuumiza
katika kipindi kilichopita.
2. Muombe Mungu au tafuta msaada wa
kisaikolojia ili uweze kuponywa moyo wako kutokana na maumivu
yaliyokupata
3. Jikumbushe kuhusu tabia, sifa na
mambo mazuri uliyonayo au uliyowahi kuyafanya.
4. Waepuke watu ambao wapo kwa ajili
ya kukuangusha au kukufanya ujione una kasoro.
5. Jikubali na ujipende, tafuta
vitu unavyovipenda kuhusu wewe, nini kinakufanya uwe tofauti na wengine?
KIMEFANYIWA
UFUPISHO NA
MWANDISHI MAGRETH GIFTH MUSHI PAMOJA NA
MABINTI WA HUDUMA YA
A LADY WITH A PURPOSE.
KWA MAWASILIANO ZAIDI
255 654 444433
@ June
2019
Download Hapa
No comments