SERVANTHOOD LEADERSHIP IN 21ST CENTURY/KIONGOZI MTUMISHI KARNE YA 21
SERVANTHOOD LEADERSHIP IN 21ST
CENTURY/KIONGOZI MTUMISHI KARNE YA 21
Kwanza kabisa Mtumishi ni kiongozi
ambaye lengo lake kubwa ni kusaidia.
Utumishi unaoongelewa hapa ni ule wa
kushirikiana na watu moja kwa moja kwenye kufanya kile mnachotakiwa kufanya.
Sio kukaa na kuagiza hiki afanye uyu alafu wewe ume relax.Ni ushirikiano wa
pande zote mbili zinazohusika hapo mbele kidogo tutaona sifa zake.
Swali ni je?Tunaweza tukapata
kiongozi wa aina hii karne hii ya 21??
Karne yenye mambo mengi na taarifa
nyingi ambazo tunaaminishwa kiongozi anatakiwa awe wa aina fulani???
Jibu ni Ndio inawezekana kabisa kuwa
na kiongozi mzuri karne hii ya 21.
Kama wakristo tunaunganishwa na
kupewa ukamilifu na Yesu unaoweza kabisa kutupa kiongozi ambaye hana sifa
potofu ambazo tunazisikia na tumezoea kusikia kwamba ni lazima kiongozi awe
nazo.
Luke 22:25_27
Akawambia wafalme wa mataifa
huwatawala na wenye mamlaka juu yao huitwa wenye fadhili. 26.Lakini kwenu ninyi
sivyo,bali aliye mdogo na mwenye kuongoza kama yule atumikaye ? 27. Maana aliye
mkubwa ni yupi? Yeye aliyeketi chakulani au yule atumikaye?Siyo yule aketie
chakulani ?Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye.
Kama Yesu mwenyewe alihudumu hata
sisi tunayo nguvu na uwezo wa kuhudumu vizuri kama Yesu alivyofanya.Kutumika ni
kazi inayotaka usiwe dictator.unatakiwa uwe tayari kuwaongoza watu. Kushirikiana
nao katika kila jambo. Tuna mfano wa viongozi ambao tumewaona
wakishirikiana na watu vizuri na kufanyika baraka.Kiongozi huyu
tunaemsaidia anaweza akawa ni kiongozi wa kuhudumu kanisani, hata sehemu
nyingine mbalimbali.
Kiongozi hatakiwi kuwa mtu wa
kuchukulia anaowaongoza advantage ( you shouldn't take advantage of the people
you are leading)
1peter 5:2 Lichungeni kundi la Mungu
lililo kwenu,na kulisimamia, si kwa kulazimishwa,bali kwa hiari kama Mungu
atakavyo, si kwa kutaka fedha ya aibu , bali kwa moyo. Ukiwa mtumishi
unayehudumu sawasawa na mapenzi ya Mungu kwako title (cheo) hakitakupa shida.
Utaichukulia kama nafasi ambayo unatakiwa kuitumia ili kutimiza mapenzi ya
Bwana.
ZIFUATAZO NI SIFA KUU TANO ZA
MTUMISHI TUNAYEMZUNGUMZIA LEO
1. Servant Heart / Moyo wa
kitùmishi
Kuwa mtumishi anayeenda na mapenzi
ya Mungu karne hii 21 unatakiwa uwe na moyo wa kitumishi.(Wito)
2. Meekness/ Upole
Hesabu 12:3
Inatuambia Musa alivyokuwa mpole
sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.Lazima utakutana na
watu wa aina mbalimbali na wenye mambo mbalimbali. Unatakiwa uwe mpole ili
kuweza kukaa sawasawa na mapenzi ya Mungu
3. Humility/ unyenyekevu
Mathayo 18:4 Basi yeyote ajinyenyekesheye
mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. Unyenyekevu
ni kila kitu. Hata Yesu alikuwa mnyenyekevu.
4. Sacrifice and selflessness/
Anayejitoa na asiye mbinafsi
Yohana 15: 13
5. Faithfulness/ mwaminifu
1korinto 4:2
Hapo tena inayohitajiwa katika
mawakili ,ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu Kiongozi lazima awe mwaminifu,Ni
vizuri ukawa mwaminifu kwa kila jambo, uhaminifu sio kwa vitu tu hata kwa watu
unaowahudumia.
Hitimisho
Utumishi ni uchaguzi(choice)Lakini
commitment inahitajika when you decide to be a leader.
1korinto 9:19
Maana ingawa nimekuwa huru kwa watu
wote, nalijifanya mtumwa wa wote ili nipate watu wengi zaidi.
Imetafsiriwa
na Dada Dorosela Kimaro.
No comments