KEYS TO GREATNESS/FUNGUO ZA UKUU.
KEYS TO
GREATNESS/FUNGUO ZA MAFANIKIO au UKUU.
Sisi sote ni watoto wa Mungu na
tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. (aliye mkuu kuliko vitu vyote).Na kwa
kila mtoto wa Mungu amepewa uwezo wa kuwa mkuu. Sisi watoto wa Mungu ni
zao/tunda la Mungu wetu aliye mkuu, na tumeumbwa kwa namna ya pekee.
Zab:139:14
"Nitakushukuru kwa kuwa
nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu yakutisha, Matendo yako ni ya ajabu na nafsi yangu
yajua sana."
UWEZO NI NINI?
NI ILE NGUVU ALIO NAYO MTU JAPO
YAWEZA KUWA HAIJATUMIKA.
Ni nguvu iliyofichika.
Ni ile namna au hali ambayo mtu
yakupasa uwe japo bado haijadhihirika katika ulimwengu wa mwili.(umbali mtu
anatakiwa kuufikia/kwenda japo bado hajafanikiwa kufika).
Tunazidi kufundishwa kuwa; Uwezo ni
yale yote Mtu anaweza kuyafanya japo bado hajayafanya/hajafikia. Uwezo si kile
Kitu mtu kashafanya LA HASHA! Kwa maana mara nyingi watu wengi huridhishwa
na kuvutiwa na yale wameshafanya/ama kufanikiwa na kusahau kuwa
wanauwezo wa kufanya makubwa zaidi.
Hivyo tukiwa tungali hai tujue kuwa tuna uwezo
wa kufanya mambo makubwa na makuu sana katika ulimwengu huu,kwa ajili ya
kizazi cha sasa na cha baadae.
Ili kuufikia ukuu/ama mafanikio yetu
makubwa funguo zifuatazo yatupasa kuzizingatia na kuzitekeleza;
UFUNGUO WA MAARIFA/UFAHAMU:
Tunaambiwa kuwa adui Mkubwa wa
mwanadamu ni ujinga na nyenzo kuu ya uharibifu wa maisha ya
mwanadamu ni ukosefu wa maarifa/ufahamu.
Hosea 4:6 maandiko yanasema;
"Watu wangu wanaangamizwa kwa
kukosa maarifa;Mimi nami nitakukataa wewe usiwe kuhani kwangu mimi;kwa kuwa
umeisahau sheria ya Mungu wako,mimi nami nitawasahau watoto wako."
Hivyo basi ili tuweze kufikia
ukuu/mafanikio katika maisha Yetu funguo ya kwanza ni maarifa,tupende kujifunza
na kupata maarifa kwa njia mbalimbali,mf kusoma vitabu na kujifunza kwa
waliofanikiwa.
Usione Shida wala aibu kuuliza
kwa kitu usichokifahamu.Kuwa na bidii katika kujifunza.Endapo Mtu utaona shida
katika kujifunza/kutafuta maarifa, usimlaumu Shetani kwa kutofanikiwa kwako
maana Huna maarifa ya kuufikia ukuu/mafanikio,wala kuanguka kwako usilaumu mtu
yeyote maana nyenzo kuu ya kuanguka kwako ni Ujinga.
TUKISOMA MAANDIKO MATAKATIFU;
Daniel 9:2 Katika mwaka wa
kwanza wa kumiliki kwake, Mimi Daniel kwa kuvizosoma Vitabu,Nalifahamu hesabu
ya miaka,ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii,ya kuutimiza ukiwa
wa Yerusalem Yaani miaka sabini.
Tunaona hapo Daniel kupitia kusoma
vitabu aliweza kupata maarifa ya kuhesabu miaka iliyobakia ya kuwa
utumwani. Kuna wakati Mwingine katika safari ya kutafuta maarifa binadamu
wanaweza kusema mengi na kuwa na maoni kadha wa kadha juu yako,LAKINI SONGA
MBELE NA USIRUDI NYUMA.
Kwa maana ni Mungu pekee ndie
anakujua wewe,hakuna binadamu anayeweza kukwambia ama kukuamlia maisha
yako.Maoni ya binadamu juu yako ni ubatili Mtupu hivyo hayawezi kubadili nguvu
na uwezo ulionao.
UFUNGUO NO.2.
KUBALI MAJUKUMU/WAJIBIKA.
Usiridhike na mafanikio ama hali
ulionayo sasa, KUBALI kuwajibika zaidi na zaidi.
Zaburi:71:21 inasema"Laiti
ungeniongezea ukuu,Urejee tena na kunifariji Moyo.
Hapo tunaona kuwa mtu anatamani kuwa
mkuu zaidi na zaidi,Hivyo usibweteke na kuridhika mahali ulipo
leo,unauwezo wa kuwajibika na kufanya makuu zaidi.
UFUNGUO NO.3
JIWEKEE MALENGO;
Tengeneza Malengo yanayotekezeka, yapange
kwa vipaumbele na uyatimize .
Weka Muda Maalumu (time frame) kwa
kila lengo lako.mf.wiki,mwezi,mwaka n.k.WEKA MIKAKATI ITAKAYOKUSAIDIA
KATIKA UTEKELEZAJI WA MALENGO YAKO KWA MAANA UKUU AMA MAFANIKIO HUWAPATA WATU
WENYE NIDHAMU NA WALIO SERIOUS NA KITU WANAFANYA AMA WANAPANGA KUFANYA. Na
katika kutimiza malengo yako hakikisha kila unachofanya unakipa umuhimu na
kutochukulia vitu as usual.
UFUNGUO NO 4.
KUMBATIA NDOTO,MAWAZO NA MAONO
YAKO.
Hapa inashauriwa usiwe kigeu geu,
Leo una kile Kesho kingine,"stick to one thing at a time" Hakuna
mafanikio au ukuu mtu anaweza kufikia bila kuwa na maono,ndoto na mawazo.Fikiria(imagine/pata
picha) kuhusu ukuu/mafanikio yako baada muda fulani Mf.unataka kuwa na
familia bora na watoto wazuri ni lazima uwe na maono na ufuatilie maono yako
hatua kwa hatua bila kuchoka wala kukata Tamaa. Mfano wa ndoto tunaona kupitia
Mwanzo 37:5-8
"Yusufu akaota ndoto, akawapa
ndugu zake habari,nao wakazidi kumchukia, akawaambia ,tafadhalini, sikieni
ndoto hii niliyoota.Tazama Sisi tulikuwa shambani tukifunga Miganda,
Kumbe!mganda wangu,ukaondoka ukasimama,Na Tazama Miganda yenu ikazunguka
ikainama mbele ya mganda wangu.Ndugu zake wakamwambia Je,kweli utatumiliki
sisi?Nawe utatutawala sisi?Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake na maneno
yake."
Tunaona Yusufu anaota ndoto ya utawala
lakini anapowashirikisha nduguze wanamchukia,Yamkini mimi na wewe tuna ndoto na
kuna watu tumewashirikisha, na badala ya kusapoti ndoto zetu wanachukia na
kutaka kutuangamiza,LAKINI NIKUTIE MOYO KUWA KILA KILICHOKIKUU HUPITIA MAGUMU.Mfano
ni dhahabu haiwezi ng'aa bila kupita katika Moto.Shikilia ndoto na maono
yako na ufanyi kazi.
FUNGUO NO.6
JENGA MAHUSIANO YENYE TIJA
Kama unataka kuwa Mkuu/kupata
mafanikio ni lazima uambatane na waliofanikiwa/waliofanikiwa, Mf.mtoto mdogo
hawezi kuwa na tabia njema endapo company anayocheza au kushinda nao hawana
maadili mazuri.
MAANDIKO MATAKATIFU;MITHALI 13:20
inasema;
Enenda pamoja na wenye hekima,nawe
utakuwa na hekima,bali rafiki wa wapumbavu ataumia. "Tunaona
maandiko matakatifu yanatuonyesha namna mtu anaweza kuwa kulingana na
watu anaoambatana nao.
Hivyo basi katika kujenga mahusiano,unayo
nafasi ya kuwa na mahusiano na watu unaowapenda na wanaokupa hamasa ya kufanya
juhudi zaidi ili kufikia mafanikio yako.
Swali la kujiuliza kabla hujaanzisha
mahusiano ama urafiki:
Kwanini uwe na mahusiano na watu
wasio na malengo yoyote katika maisha? Kwanini uwe na mahusiano na mahusiano na
watu wanaotaka kubaki kama walivyo /wameridhika?
Maandiko(Mithali 27:17) pia hapa
yanasema"Chuma huona Chuma, Ndivyo mtu auonavyo Uso wa rafiki yake."Wapendwa,nataka
leo tuanze kufanya tathmini juu ya marafiki tulionao, hata ikitubidi kubadili
uelekeo kwa ajili ya marafiki zetu.
UAMINIFU.
Hapa tunahimizwa kuwa waaminifu na
kile unachotamani kuwa.
Mfano;kwa Mtu Anayetamani kuwa
mwandishi Mashuhuri wa vitabu ili aweze kufikia hicho anachotamani cha kwanza
ni lazima awe na Imani itakayomsukuma kufanya bidii katika kufikia hiyo level
anayotamani awe.MAANDIKO MATAKATIFU KUTOKA MARKO:9:23 inasema"Yesu
akamwambia Ukiweza!Yote yawezekana kwake aaminiye."
MARKO 10:27 "Yesu akawakazia
macho akasema,kwa wanadamu haiwezekani bali kwa Mungu sivyo, maana yote
yawezekana kwa Mungu."
Maandiko haya yanatuonyesha jinsi
Imani yako ni nyenzo kuu katika kufikia chochote unachotamani kuwa.Maana Imani
uliyo nayo ndio ikupayo nguvu ya kutenda na kujitoa zaidi.
UFUNGUO NO.7 HUDUMIA/FANYA
HUDUMA.(SERVICE)
Huwezi kuwa mkuu ama kufanikiwa hadi
pale utakapojitoa kwa ajili ya wengine.MAANDIKO YAMETUONYESHA MFANO MINGI,juu
ya watu waliojitoa na kufanya huduma na ndipo walipokuwa wa kuu. Yusufu
alikuwa kijakazi hatima yake ilikuwa ni Uwaziri.Saul alimhudumia babae. Elisha
alimhudumia Bwana wake Eliya.Yesu Kristo Mwenyewe alijitoa kwa Mungu baba na
kwa wanadamu pia na ndipo alipokuwa Mkombozi wa ulimwengu.
Hivyo katika kutoa huduma kwa
uaminifu na moyo mkuu yamkini ndipo muujiza wako ulipo,fanya jitihada katika kuwahudumia
wengine haijalishi utakutana na magumu yapi ama gharama kubwa kiasi gani,maana
pia katika huduma ndipo Unyenyekevu wako utapoongezeka na penye Unyenyekevu siku
zote Pana mafanikio makubwa.
UFUNGUO 8.TOA SHUKRANI.
Katika Maisha yako na safari yako ya
mafanikio,jifunze kutoa Shukrani,kwanza kwa Mungu wetu kwa jambo lolote Liwe
jema ama baya
Pili kwa wanadamu waliokushika mkono
kwa namna yoyote ile,Neno ASANTE lina nguvu sana wapendwa,na kama haujawahi
kulitumia au linakuwa gumu kwako jifunze kuanzia Leo. pia kuna namna
mbalimbali za kutoa shukrani zako na shukrani ni njia ya kuomba tena na
tena,Hivyo basi tunahimizwa kuwa watu wa shukrani ili kufikia mafanikio
yetu katika maisha.
IN SUMMARY;FUNGUO ZA MAFANIKIO YAKO:
TAFUTA MAARIFA.
WAJIBIKA/KUBALI MAJUKUMU.
WEKA MALENGO.
KUMBATIA NDOTO,MAWAZO NA MAONO YAKO.
KUWA NA IMANI.
JENGA MAHUSIANO YENYE TIJA.
TOA HUDUMA/HUDUMIA.
Imetafsiriwa na Dada FLORA MASHIMBA
Asante mtumishi Magreth kwa kushare. Mungu akaibari kazi ya mikono yako ukainuliwe kwa viwango vingine. Utukufu hadi utukufu.
ReplyDelete