MSICHANA MWOMBAJI NA MCHA MUNGU
Msichana
unapaswa kuwa na tabia ya kuomba na kutafuta kuwa rafiki wa Mungu. Haya yanapaswa
kuwa ndio maisha yako ya kila siku na sio matukio ya muda hasa ukiwa na shida.Usiombe
pale tu unapoona mambo hayaendi sawa, hapana unatakiwa uwe mwombaji wa kila
wakati na binti anayetafuta kufanya mapenzi ya Mungu nyakati zote, hii ndio
tabia ya kiungu katika maisha ya binti aliyeokoka.
Kuna vitu vingi sana
hautaweza kuvipata kama hauombi na kama una konakona kwenye maisha yako. Na
tambua kuwa baraka zako nyingi zipo magotini mwako na katika kumuishia Mungu (utakatifu),
ni jukumu lako sasa kuingia magotini na kumwomba Mungu akusaidie kumtii Roho
wake Mtakatifu anapokufundisha na kukushauri.Unapokuwa muombaji kuna vitu vingi
Sana vitatendeka katika maisha yako na pia kuna mazingira ambayo Mungu atakuwa
anakuepusha nayo kwani mwili wako unakuwa unahuishwa chini ya Mungu (Warumi 12;
1).
Mwanamke
amchae Mungu ndiye atakayesifiwa.Mith 31; 10 Biblia imeshatupa muongozo hapa kuwa mwanamke anayemcha na
kumsikiliza Mungu atasifiwa, kamwe mwanamke anayekaa na mashoga zake tu na
kujadili mambo yasiyo na maana hatosifiwa daima, zaidi sana ni kujikuta unapata majeraha ya nafsi , viwango vyako viweke kwa Yesu
pekee.
No comments